KAMPUNI ya TOLGases Ltd inatarajia kuongeza uzalishaji wa gesi ‘Oxygen’ zinazotumika katika hospitali baada ya kununua mtambo mpya na kuzima wa zamani.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya gesi, Daniel Warungu, ameyasema hayo leo Agosti 28, 2020 katika wa mkutano wa  mwaka  wa  wanahisa uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Warungu, amesema mtambo huo mpya utaingia nchini mwezi ujao na kuanza kazi mara moja. 

Alisema waliamua kuzima mtambo wa zamani ulikuwa unawapa hasara ya bilioni 1.2 kwa mwaka ya umeme pekee bila uzalishaji mzuri na kuifanya kampuni isiaminike.

 Warungu ameeleza kuwa ujio wa mtambo huo mpya utaondoa tatizo la gesi katika hospitalini zote na gawio kwa wanahisa litaongezeka tofauti na mwaka uliopita.

"Sababu ya usumbufu wa umeme ulikuwa ukikatika hata dakika Moja unapata hasara, kwa wastani tulikuwa tunatumia mpaka milioni 150 kwa mwezi lakini sasa tumepunguza hadi milioni 13 hadi14 kwa mwezi ambapo ni punguzo la asilimia kama 90." Amesema  Warungu

Amesema, tatizo hilo la mtambo pia lilikuwa likiwaletea shida kwenye masoko  kwa kutoaminika kwa sababu leo una gesi kesho hauna, kitendo kilichopelekea bodi ya wakurugenzi  kuamua kuuzima ule mtambo na ununuliwe mtambo mpya ambao unatarajiwa kuingia kuanzia mwezi ujao na mpaka kufikia mwisho wa mwaka mtambo wote utakuwa umekamilika.

"Kuanzia mwaka ujao tunatarajia hatutakuwa na mtambo wenye hasara, tunataraja gawio litaongezeka sababu mitambo yetu yote itakuwa inajiendesha kwa faida, kitu ambacho kitawafurahisha wanahisa wetu kuanzia mwaka ujao TOLs. Itakuwa Bora zaidi na gesi."

“Kuanzia mwakani Tanzania itakuwa haina tatizo la Oxygeni katika hospitali, tumejikita  zaidi katika hospitali kwa sababu ndiyo kuna mahitaji makub  wa ya wagonjwa,” amesema Warungu

 Aidha amesema kutokana changamoto zilizojitokeza za mtambo huo, pamoja na kununua mwingine wa muda, mwaka huu faida ilishuka.

“Mtambo wa mbadala tulionunua ulitusaidia hasa kipindi cha mshtuko wa janga la Corona, tulikuwa tunasambaza gesi vizuri hakukuwa na shida.” AmesemaWarungu.

Naye Mjumbe wa Bodi ya kampuni hiyo, Simon Mponji, akizungumza kwa niaba ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Michael Shirima, alisema watahakikisha wanaongeza mapato na hesabu zinawasilishwa vizuri. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...