NA KHALFAN SAID, NYAKABINDI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambako kiongozi huyo amefika kufungua rasmi maonesho ya mwaka huu ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo.
Makamu wa Rais alipokewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Y. Kibesse na Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo ambapo alitembelea idara mbalimbali za Benki hiyo na kuelezwa jinsi zinavyowahudumia wananchi wanaofika kwenye banda hilo.
Maonesho ya mwaka huu ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020."
Lengo hasa la maonesho hayo yanayofanyika kitaifa kwa mara ya tatu mfululizo kwenye viwanja hivyo ni kutoa fursa kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia Bora za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija na uhakika wa chakula, kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto), akimsikiliza Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT, Bi. Vicky Msina (katikati) huku Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse (kulia) akishuhudia wakati Kiongozi huyo alipotembelea banda la Benki Kuu kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo nya mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambako maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu wa 2020 yanafanyika. Makamu wa Rais alitarajiwa kufungua rasmi maonesho hayo.
 Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo (kushoto) akimuongoza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kutembelea banda hilo.
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akipokea mfuko wenye machapisho mbalimbali yanayoelezea shughuli za BoT kutoka kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Kibesse wakati alipotembelea banda hilo leo Agosti 1, 2020
Makamu wa Rais akiondoka wkenye banda la BoT baada ya kulitembelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...