Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia moja ya dawa za mifugo katika kiwanda cha Farm Accesses Ltd cha mjini Arusha inachotengeneza pembejeo za mifugo. Waziri Mpina alitembelea kiwanda hicho jana akiwa katika ziara ya kikazi

Waziri Luhaga Mpina, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha naKilimanjaro aliambatana na wajumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank yaMaendeleo ya Kilimo Bw. Japhet Justine (kushoto)

Waziri Luhaga Mpina katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro na Arusha
Msajili wa bodi ya nyama kutoka katika Wizara ya Mifugo na UvuviBw.Imani Sichwale alikipongeza kiwanda cha Meat King kwa kuzalisha nyamazilizo katika kiwango cha hali ya juu.
Na Mwandishi wetu, Arusha.
Waziriwa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wawekezaji katika sekta ya
Mifugo husasani wamiliki wa viwanda vya nyama nchini kutafuta masoko ya
uhakika ndani na nje ya nchi.
Waziri Mpina aliyasema hayojijini Arusha alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea
viwanda vya mazao ya mifugo ambapo alisema Serikali inawaunga mkono wawekezaji katika sekta ya nyama na kushauri wafanye upanuzi wa viwandavyao kwani baada ya janga la covid 19 biashara sasa imeanza kurudivizuri.“Changamkieni masoko na ziwepo products zote katika masoko ya ndani watanzani na wageni wanahitaji wazipate.”Alisisitiza.
Akiwakatika kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat king mjini Arusha Mpinaaliwataka wafanye bidii katika kuhakikisha wanapata watu wanaowezakuyafikia masoko kwa kwenda au kuwatumia mawakala hasa katika mikoa yaMwanza, Tanga na sehemu nyingine za nchi.
Katika ziara yakekiwandani hapo Waziri Mpina, aliishauri Bank ya Maendeleo ya Kilimo TADB
kuangalia uwezekano wakupanua wigo wa mikopo ili viwanda viendelee kuwepo sambamba na kuinua soko la ndani na kuimarisha mnyonyoro wathamani wanyama na kufanya bidhaa hizo ziwe na ushindani kimataifa,kutoa ajira kwa watanzania na wafugaji wazidi kuinuliwa kiuchumi.
Akiongeakatika ziara hiyo ya Waziri Mpina, Kaimu Mkurugenzi wa mikopo nabiashara kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Jeremiah Muhanda,alisema Bank hiyo imeweza kuwasaidia wawekezaji kupata ,machine zakisasa, mitaji yakufanyia kazi na kuwasaidia mitaji wafugaji kupitia
vikundi.
Na aliongeza kwa kusema kuwa Bank hiyo pia imewezeshakiwanda cha pembejeo za mifugo cha farm access cha mjini Arusha mkopo wakiasi cha shilingi milioni mia nne tisini na tisa (499Milioni).
Kwaupande wake Msajili wa Bodi ya nyama nchini Bw. Imani Sichalwealikipongeza kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat King kwa kuzalishanyama yenye viwango vya juu ambapo awali ilikuwakiagizwa kutoka nje yanchi.
Alipokuwa katika kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro FreshWaziri Mpina alimpongeza muwekezaji huyo kwa kununua maziwa kwawafugaji kwa bei nzuri ya shilingi mia nane themanini (880/-) kwa litaikiwemo kuwapongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuzalisha lita elfu nane (8000) mpaka elfu tisa(9000)kwa siku na maziwa hayo kufika katika kilamaeneo nchini.
“Serikali itaendelea kuunga mkono na kusaidiakutatua changamoto zozote na msipate vikwazo kwenye soko zuri lawafugaji wetu, ilikuweza kupata maziwa mazuri na bora...Nawasihi pia mpanue masoko kadiri mnavyoweza, nawahakikishia masoko yaliyopoyataendelea kulindwa.” Alisema.
Aidha,Waziri Mpina alielekezabodi ya maziwa kufuatilia maziwa yanayoingizwa toka nje ya nchi kinyumena utaratibu yaondolewe na walipe kodi za serikali na nchi isiwe dampola kuingiza bidhaa hizo kinyume nataratibu.
Alipotembelea kiwandacha nyama cha Elia Foods Overseas ltd kilichopo Wilayani Longido,Waziri Mpina alimpongeza muwekezaji huyo kwa kufanya uamuzi wakujenga kiwanda hicho nchini.
Hatahivyo muwekezaji huyo alimuomba Waziri Mpina kushugulikia changamotoya kodi anayokabiliana nayo ili kuweza kuingiza vipuri toka nchi jiraniya Kenya na kuanza uzalishaji kwawakati, ambapo katika hilo WaziriMpina alielekeza dawati la sekta binafsi la wizara yake kushughulikiachangamoto hiyo mara moja ili uzalishaji katika kiwanda hicho uanze.
Ziaraya Waziri Mpina Mkoani Arusha ilihusisha kiwanda cha kuchakata nyamacha Meat King, Elia Foods Overseas ltdnakiwanda cha maziwa chaKilimanjaro Fresh.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...