Mgombea ubunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (Simba wa
Manyara) akiwapungia mkono ili kuwasalimia wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) alipofika kuchukua fomu ya kuomba kuteulia kugombea
ubunge.

****************************
Na Mwandishi wetu, Simanjiro.
CHRISTOPHER Ole
Sendeka (Simba wa Manyara) aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Simanjiro kwa
miaka 10 mfululizo kutoka maka 2005/2015 ambaye alishinda kura ya maoni
hivi karibuni na jina lake kurudisha na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
amechukuwa fomu ya kugombea ubunge huo huku akisindikizwa na maelfu ya
wanachama wa chama hicho.
Ole Sendeka huku
akiwa na msafara wa magari na pikipiki amepokelewa kwa maandamano na
kuahidi kuwatumikia wananchi wa eneo kwa uaminifu na uadilifu endapo
atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Akizungumza na
wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet baada ya kuchukuwa fomu amesema
anatambua wananchi wa eneo hilo wana kiu kubwa ya kupatiwa maendeleo
hivyo atajitahidi kuhakikisha anatimiza suala hilo.
Amesema muda wa
kampeni ukifika atazungumza maendeleo yote wananchi wanayotarajia
ikiwemo barabara ya lami ya Kia-Mirerani-Orkesumet na kukamilishwa kwa
mradi mkubwa wa maji wa Ruvu Orkesumet.
“Nawashukuru sana
kwa ninyi kunisindikiza kuchukua fomu kwani mmekuja kwa wingi na
nawashukuru sana ila wote tuwe mabalozi wazuri wa Rais John Magufuli
kuhakikisha anachagulia kwa kura nyingi za kishindo,” amesema Ole
Sendeka.
Mwanachama wa CCM
wa kata ya Terrat, Baraka Mollel aliishukuru NEC kwa kurudisha jina la
Ole Sendeka ambaye wajumbe wa CCM wa wilaya ya Simanjiro walimchagua kwa
kura 306 hivyo kushika nafasi ya kwanza.
“Tunamshukuru
Rais Magufuli kuturudishia Simba wa Manyara kwani wananchi wa Simanjiro
bado wanampenda na wanahitaji kutumikiwa na Ole Sendeka katika kipindi
kingine cha miaka mitano,” amesema Mollel.
Hata hivyo,
Katibu wa CCM wilaya ya Simanjiro, Ally Kidunda amewataka wanachama wote
wa CCM waliochukua fomu za kugombea na majina yao kutorudi wavunje
makundi na kumuuza mgombea mmoja wa CCM aliyeteuliwa.
“Pamoja na hayo
nawasihi wanachama wa CCM acheni tabia za kuzodoana na kutoleana maneno
ya kashfa kwa wale alioshinda na kushindwa kwani hivi sasa tunatetea
chama chetu siyo mtu,” amesema Kidunda.
Kwa upande wake,
msimamizi wa uchaguzi huo, Yefred Myenzi amesema hadi hivi sasa wagombea
wawili Ole Sendeka wa CCM na Emmanuel Landey ndiyo wanachama wa vyama
vya siasa waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.
Myenzi amesema
atashirikiana na maofisa watano wa ofisi yake katika kuhakikisha
shughuli ya uchaguzi mkuu unafanyika kwa haki na kufuata kanuni,
taratibu na sheria za uchaguzi zilizoeka kikatiba kupitiaTume ya Taifa
ya uchaguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...