Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wananchi wa kijiji cha Rungemba wakati wa ziara ya kukagua miradi pamoja na kusikiliza kero za wananchi
Stephen Kalinga akiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru akamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara
Stephen Kalinga na mwenzake wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru wakamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara
Na Fredy-Mgunda,Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameamuru kukamatwa kwa mwenyekiti wa bodi ya maji ya kijiji cha lungemba wilayani mufindi Stephen Kalinga kwa kosa la kuwamchonganishi baina ya serikali na wananchi huku akiahidi kuchangia mifuko 100ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi la akinamama.
Akisikilizakero za wananchi wa kijiji hicho,mkuu wa mkoa alipokea barua kutoka kwamwananchi iliyokuwa inatuhuma kwa baadhi ya viongozi wa kijiji hicho na kuanzakuzitafutia majibu kwa viongozi waliokuwa wametajwa.
Lakinimkuu wa mkoa Ally Hapi alimvua cheo cha kuwa mwenyekiti wa kamati ya maji yakijiji hicho na kuteua kiongozi mwingine wa muda hadi pale mkutano wa kijijiutakapopitisha jina la kiongozi mpya.
Hata hivyoviongozi wa kijiji kijiji hicho na wananchi walimuunga mkono mkuu wa mkoa wa IringaAlly Hapi kwa uamuzi wa kumvua vyeo bwana Stephen Kalinga kwa kuongea uongoambao ulitaka kuvuruga amani ya wananchi wa kijiji cha Rungemba.
Hapialiongeza kwa kusema kuwa wananchi watakiwa kuendelea kujitolea katika shughuliza kimaendeleo kama kuiboresha zahanati hiyo hadi kufikia hadhi ya kuwa kituocha afya lengo kuu likiwa ni kuendelea kuboresha sekta ya afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...