Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
KATIKA wiki iliyoishia Agosti 21 mwaka huu, Thamani jumla ya Miamala ya hisa na Hatifungani zilizonunuliwa na kuuzwa katika soko la hisa ilikuwa Sh. bilioni 63.77 kati ya hizo Sh bilioni 1.29 ilikuwa ni upande wa hisa ni Sh.bilioni 62.48 ikiwa ni Hatifungani.
Hayo yamelezwa leo jijini Dar es salaam leo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam Moremi Marwa wakati wa akitoa ripoti ya wiki hiyo ambapo amesema ukwasi katika segment ya hisa ilipungua kutoka Sh.bilioni 13.23 katika wiki iliyoishia August 14 hadi Sh. bilioni 1.29 wiki iliyoishia Agosti 21 mwaka huu.
Aidha amesema ukwasi uliongezeka kutoka shilingi bilioni 57.71 hadi kufikia shilingi bilioni 62.48.Hata hivyo amesema katika mchanganuo wa mchango wa Kampuni Kaunta ya TCC ndiyo iliyoongoza kwa kuchangia Thamani ya Mauzo kwa kiwango cha Asilimia 81 ikifuatiwa na CRDB kwa asilimia 13.
Ameongeza kuwa thamani ya jumla ya ukubwa wa soko uliongezeka kwa kiwango cha billion 201 kutoka shilingi trilioni 14.51 wiki iliyoishia Agosti 14 mpaka kufikia Sh.trilioni 14.72 wiki iliyoishia Agosti 21 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 1.4.
Aidha amesema hiyo ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya kaunta za CRDB asilimia 12 ,KCB asilimia 2 na NMG asilimia 7 lakini haikuondoa Punguza lilisababishwa na kaunta zingine.
Sambamba na hayo thamani ya ukubwa wa soko la ndani uliongezeka kwa kiwango cha Sh.bilioni 13 kutoka shilingi trilioni 9.157 wiki iliyoishia Agosti14 hadi kufikia thamani ya mtaji ya Sh.trilioni 9.17 katika wiki iliyoishia Agosti 21 mwaka huu. Amesema hiyo ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya CRDB ambayo ilipanda kwa asilimia 12.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa soko la hisa Dar es Salaam, Moremi Marwa akizungumza na waandishi wa habari hawapp pichani alipokuwa akitoa ripoti ya wiki ya hisa na hatifungani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...