Msimamizi wa
Uchaguzi wa Jimbo la Nzega Mjini Philemon Magesa alifungua jana mafunzo
ya siku tatu ya wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata.

Hakimu Mkazi
Mwandamizi Mfawidhi wilaya ya Nzega Glays Barthy akitoa maelekezo ya
kuzingatia jana kwa Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata za Jimbo la Nzega
Mjini.


Hakimu Mkazi
Mwandamizi Mfawidhi wa Wilaya ya Nzega Glays Barthy awaapisha wasimamizi
wasaidizi ngazi ya Kata za Jimbo la Nzega Mjini.
……………………………………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT
MSIMAMIZI wa
Uchaguzi wa Jimbo la Nzega Mjini Philemon Magesa amewataka Wasimamizi
wasaidizi ngazi ya Kata kuepuka ushabaki wa aina yoyote wa kisiasa
katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutosababisha vurugu wakati zoezi
la uchaguzi mkuu ujao.
Alitoa kauli
hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi
Mkuu ujao kutoka Kata 20 za Halmashauri hiyo.
Magesa
alisema ili Wasimamizi wasaidizi wawe salama katika zoezi hilo ni vema
wakazingatia Katiba , Sheria na Kanuni zinasimamia zoezi zima la
uchaguzi.
Alisema hali
hiyo itasaidia kuufanya uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo
kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
Aidha Magesa
aliongeza kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni muhimu
wakavishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika
masuala ambayo wanastahili kushirikishwa.
Naye Hakimu
Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Glays Barthy walioteuliwa na Ttume ya Taifa ya
Uchaguzi(NEC) ambao ni wanachama wa vyama vya siasa kuhakikisha
wanajitoa katika vyama vyao ili kuweza kusimamizia zoezi kwa umakini.
Aliwataka
wasimamizi wasadizi hao kuwa makini na watu wa karibu nao kwa kujiepusha
kutoa maoni ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa sheria za uchaguzi
na kanuni zake.
“Muwe makini na
ma group mnayo socialize kwa kuepuka kutoa maoni ambayo nanaweza
kusababisha kuonekana unashabikia upande fulani na kusababisha vurugu”
alionya.
Alisema katika
kipindi chote cha zoezi la uchaguzi wanapaswa kujizuia kupenda
kujadiliana na makundi mbalimbali nyakati zote za shughuli za uchaguzi.
“Tunajua baadhi
yenu mna kazi za vyama vya siasa …baada ya kiapo hiki mnatakiwa kujitoa
kabisa kuzungumzia mambo ya vyama vyenu ili muweze kuwatendea haki hata
wote…na wale wenye ushabiki wa ndani ni vema wakaauacha ili waweze
kutekeza majukumu yao kwa mujibu Katiba, Sheria na kanuni zinazosimamia
uchaguzi” alisisitiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...