Naibu waziri wa
Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Viongozi wa mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuhakikisha kuwa wananunua Viatu kutoka
kiwanda Cha Kilimanjaro Leather Industries Co. ltd ,kilichopo Moshi
katika Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na
wananchi wa Kanda ya Kaskazini katika Viwanja vya Themi Njiro Nane
Nane,Ulega alisema kuwa ni lazima viongozi wa mikoa hiyo wawe mfano wa
kuweza kuratibu na kununua viatu katika kiwanda hicho.
Alisema
kuwa kiwanda hicho kimejengwa na Serikali kwa shilingi bilioni 69,ambao
Raisi dkt.John Pombe Magufuli alitoa fedha hizo ili kuhakikisha
Kiwanda hicho Cha kuchakata ngozi na kuzalisha bidhaa nyingine Mbali Mbali za ngozi kinajengwa hapa nchini.
Aidha
Ulega alisema kuwa kwa kuwa kiwanda cha Karanga kitakuwa na uwezo
mkubwa wa kuzalisha Viatu Hadi kufikia jozi milioni 1.5 kwa Mwaka,hivyo
Watanzania kutumia bidhaa hizo haswa Viatu.
"Nawataka ninyi
viongozi mliopo hapa wa mikoa hii ambao mmesifiwa Sana hapa na Mkuu wa
mkoa wa Arusha Idd Kimanta kuwa mpo vizuri,ratibuni hakikisheni kuwa
msimu wa January mwakani watoto wetu wa mikoa hii wanavaa Viatu vya
kiwanda hiki,kwanza vina ubora,bei zake ni nafuu na ni bidhaa kutoka
kwetu,muone fahari ndugu zangu Watanzania mfano huu uanzie Sasa hapa
Kaskazini."alisema
Ulega.
Alitoa Rai kwa viongozi kulinda
viwanda vya ndani kwa kuhakikisha kuwa wanavitembelea mara kwa
mara,kuvitizama na kuangalia changamoto zilizopo na kuzitatua ili
vifanye uzalishaji wao vizuri.
"Hakikisheni kuwa kazi hii
mnanifanya wenyewe msisubirie waje watu kutoka nje ili waweze kuwafanyia
Mambo yenu,tuvilinde tulivyonavyo ili viweze kutusaidia na
kutusitiri,pamoja na kukuza Uchumi wetu."alisema Ulega.
Nae Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti aliwataka wakulima,wafugaji na
wavuvi kuhakikisha kuwa wanatumia maonesho hayo kuweza kutambua mchango
wa taasisi Mbali Mbali za fedha ili wazitumie kukuza shughuli zao.
"Taasisi
hizi za fedha zimekuwa Ni changamoto kwa Makundi haya Sasa tumezileta
hapa ili wakulima,wafugaji,na wavuvi waweze kufanya vyema na kukuza
Uchumi wao."alisema Mkirikiti
Maonesho ya 27 ya Kilimo na Mifugo
na Uvuvi yanahitimishwa leo August 10 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema kuwa"Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi
Bora 2020."Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisikiliza maelekezo ya
mkulima katika Viwanja vya Themi Njiro Nane Nane Mkoani Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...