Na Woinde Shizza,Michuzi TV Arusha
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameagiza kufutwa Mkataba wa kazi wa Mkandarasi, kutoka kampuni ya M/s Nipo Group Limited, aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza mkoani Arusha, kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

Aliyasema hayo Jana kwa Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kijijini Lendkinya, Kata ya Sepeko, wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha.

Dkt Kalemani alitoa maelekezo hayo baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika maeneo kadhaa ya Wilaya ya Monduli, ambapo alibaini kuwa Mkandarasi husika ametelekeza kazi hiyo kwa muda mrefu wà kipindi Cha zaidi ya miaka mitatu, akiacha nguzo zilizosimikwa pasipo kuvuta nyaya wala kuunganisha umeme.

Akizungumza na wananchi wa Lendikinya, Waziri aliwaeleza kuwa Mkandarasi husika alianza kazi hiyo tangu mwaka 2018 na alipaswa akamilishe mwishoni mwa June 30 mwaka huu, lakini utekelezaji wake unasuasua ambapo tangu mwezi was sita hajaonekana kazini.

Aidha Waziri pia alielekeza Mkandarasi huyo akatwe asilimia 10 ya malipo yake kutokana na kuchelewesha kazi ambapo alisisitiza tanesco na REA kufuata Sheria za kimkataba pamoja manunuzi katika kukatisha mkataba huo

Akiendelea kutoa maelekezo, Waziri aliwataka TANESCO na REA kumpatia kazi hiyo Mkandarasi mwingine mwenye uwezo au ifanywe na TANESCO wenyewe na kuhakikisha inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba, mwaka huu.

Katika hatua nyingine Waziri aliagiza kukamatwa na Polisi, kuwekwa ndani na kuhojiwa Mwakilishi wa Mkandarasi huyo aliyekuwepo katika ziara ya Waziri aliejulikana kwa jina la Magesa Shija ili atoe maelezo kuhusu pesa ambayo Serikali imelipa kwa kazi husika, imetumika vipi huku alisisitiza wakati muwakilishi huyo akiwa Ndani wakurugenzi wa Nipo wasakwe na wakamatwe kwaajili ya kutoa maelezo

Aidha alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Edward Balele kutumia Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwakamata Wakurugenzi wa Kampuni husika ambao hawakushiriki katika ziara hiyo, ili wahojiwe walikopeleka pesa ya Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele alimpongeza Dkt Kalemani kwa ufuatiliaji makini wa kazi ambao umemwezesha kubaini udhaifu wa Mkandarasi husika na kuchukua hatua stahiki zinazolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kama Serikali ilivyodhamiria.

Mkandarasi amefikia asilimia 65 ya kazi husika ambapo kwa mujibu wa Mkataba, alipaswa kuwa amefikia asilimia 92 hadi sasa kwa malengo ya kukamilika Agosti 30, mwaka huu.

Alimshukuru kwa niaba ya wananchi mwenyekiti wa Kijiji Cha Lendkinya Olais Saribabi alimshukuru Waziri kwa hatua aliowachukulia wakandarasi hao kwani wamekaa mda mrefu wakiwa wanaona nguzo lakini umeme hawana.

Alisema kutoka na kazi alizofanya Rais anahaidi kumpa Kura kwa kishindo.
Waziri wa nishati Merdad Kalimani akiozungumza na wananchi wa kata ya Sepeko iliopo wilayani Monduli mkoani Arusha juzi wakati alipotembelea katika kata hiyo kukagua Mradi wa Rea unaotekelezwa katika vijiji 62 vilivyoko katika Wilaya hiyo.
Waziri wa nishati medardi Kalimani wa kwanza kushoto akimuliza swali Mhandisi wa kampani ya Nipo Group wa kwanza kulia Magesa Shija juzi alipofanya ziara ya kutembelea Kijiji Cha Lendkinya kuangalia na kukaguwa Mradi wa umeme vijijini Rea 3 ambapo alimsimamisha mkandarasi wa kampuni hiyo baada ya kushindwa kumaliza mkataba Ndani ya muda uliopangwa.
(Picha na Woinde Shizza,Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...