
SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO) limeripoti idadi kubwa ya visa vya virusi Corona ulimwenguni na visa 307,930 vimethibitishwa kwa siku moja.
Jimbo Victoria ni la pili lenye idadi kubwa ya watu nchini Australia na kitovu cha mlipuko wa virusi Corona nchini humo,
Vimeripotiwa visa 35 vipya ambavy ni ongezeko la chini zaidi la kila siku katika miezi mitatu.
Zaidi ya watu milioni 28.9 kote ulimwenguni wamegundulika kuwa na virusi corona na zaidi ya 922,000 wamefariki duni, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Karibu watu milioni 19.5 wamepona.
Janga la Corona lilikumba dunia mnamo 31 Desemba 2019, inayojulikana rasmi kama COVID-19. Virusi vilitengwa kwa mara ya kwanza na watu wenye homa ya mapafu katika mji wa Wuhan, nchini China.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...