Mhadhiri wa chuo kikuu cha sayansi na teknologia cha Nelson Mandela, Profesa wa hisabati Verdiana Grace Masanja, ameyasema hayo kwenye mahafali ya 11 ya shule ya sekondari Star High school ya Mbuguni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Prof Masanja amesema wasichana wakipewa kipaumbele kwenye elimu sawa na wavulana, Taifa kwa ujumla litanufaisha, kwani mwanamke ndiyo mtu wa kwanza kuwa karibu na familia.
Amesema hata kwenye shule bora na zenye vipaji inaonyesha msichana hapewi kipaumbele kama wanavyopewa wavulana hivyo jamii inapaswa ibadilike.
"Tuwekeze kwa wasichana kwenye elimu na tuwape nasaha za kujichunga kwani njia ya binti ni ngumu kuliko mvulana kuna vishawishi vingi hadi afauli,' amesema Prof Masanja.
Mkuu wa Star high school, Sister Monica Massawe amesema shule hiyo ilianzishwa na shirika la kimisionari la Mitume wa Yesu, Januari 20 mwaka 2007.
Mkurugenzi wa STEMM, John Lidgett amewapongeza walimu na uongozi wa shule hiyo ndiyo sababu shirika hilo lina watoto 10 wanaosoma hapo Star high school.
Mkuu wa shule ya sekondari Star High school iliyopo Kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, Sister Monica Massawe akizungumza kwenye mahafali ya 11 ya shule hiyo.
Mhitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Star High school iliyopo Kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, Evaline Kilonzo akikabidhiwa zawadi ya cheti cha ufaulu somo la sayansi na mgeni rasmi wa mahafali ya 11 ya shule hiyo, Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Sayansi na Teknologia cha Nelson Mandela, Profesa wa hisabati, Verdiana Grace Masanja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...