……………………………………………………………………
Na.Mwandishi Wetu,Mwanza
Kocha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mpambano wa kesho dhidi ya Yanga na kwamba anaimani ataibuka na ushindi mnono katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Habibu amesema kuwa
hadi Sasa ameshafanya maandalizi ya kutosha na kwamba hanahofu na mchezo
huo kwakuwa anakikosi kipana na kwamba silaha alizonazo zinatosha
kuiadhibu Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Ameongeza kuwa licha
ya kwamba kikosi hicho hakikuweza kufanya vizuri katika michezo kadhaa
iliyopita lakini tayari ameshazifanyia kazi changamoto zilizopelekea
kupoteza kwa michezo hiyo.
” Tumekuja mwanza
kutafuta alama 9 katika michezo mitatu tuliyonayo, kesho tunachukua
alama tatu kwa Yanga halafu tunaenda kuchukua kwa Gwambia, Biashara na
hivyo tukirejea Jijini Dar es Salaam tunarudi kwa kishindo kutokana na
ushindi ambao tutakuwa tumeupata” amesema Kocha Habibu.
KMC FC kesho inacheza
mchezo wake wa mzunguko wa nane katika msimu wa Ligi kuu soka Tanzania
Bara dhidi ya Yanga na kwamba kikosi chote kipoimara katika mpambano huo
sambamba na wachezaji kuwa na morali nzuri ya mchezo.” ameongeza Kocha
Habibu.
Wakati huo huo Afisa
Habari na Mahusiano wa Timu hiyo ,Christina Mwagala amesema kuwa katika
mchezo huo wamejipanga vizuri katika suala zima la uuzwaji wa Tiketi na
kwamba hakutakuwa na changamoto zozote katika mchakato huo.
Ameongeza kuwa katika
kuhakikisha kuwa mpambano huo unakuwa mzuri, uongozi umejipanga na
kwamba mageti yote yatakuwa wazi kuanzia saa 1.00 asubuhi na hivyo kila
geti litakuwa na wahusika wanaokata Tiketi hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...