Na Lusajo Frank DSJ
RAIS wa zamani Burundi, Pierre Buyoya amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila yeye mwenye kuwepo katika hukumu ya mauaji ya mtangulizi wake, Rais wa nchi hiyo Melchoir Ndadaye mwaka 1993.
Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama ulioonyeshwa kwa shirika la habari la AFP, Buyoya alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Rais wa Burundi ambaye alichaguliwa kidemokrasia katika nchi ya Burundi.
Ndadaye, wakati huo aliondolewa madarakani baada ya kuitumbukiza serikali yake vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Tofauti na Buyoya, maafisa wengine 18 waandamizi wa kijeshi na raia wa Burundi walikuwa karibu naye wamepewa hukumu ya kifungo Maisha Jera.
Wengine watatu wamehukumiwa miaka 20 jela kwa Uzembe katika uhalifu.
Ingawa Waziri mkuu wa zamani wa Burundi, Antoine Nduwayo, alifutiwa mashitaka baada ya kukutwa hana hatia kwa sababu hakuhusika na mauaji hayo.
Watu watano kati ya walioshitakiwa ambao walikuwa mahakamani, na wengine walihukumiwa licha ya kutokuwepo mahakamani.
Buyoya kwa sasa ni mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Mali na ni kiongozi anayeheshimika barani Afrika pamoja na mataifa ya kigeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...