
RC Kunenge amesema kwa Sasa serikali kwa kutumia TARURA na TANROAD inaendelea kukarabati miundombinu yote iliyoathiriwa na mvua ikiwemo barabara, Mifereji, mito, umeme na miundombinu ya maji ili huduma ziweze kurejea Kama awali.
Aidha RC Kunenge ametoa pole kufuatia vifo vya watu 12 vilivyojitokeza kutokana na mvua ya juzi ambapo amesema mbali na vifo hivyo pia zaidi ya nyumba 800 ziliathiriwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi.
Pamoja na hayo RC Kunenge ameeleza kuwa Kamati za maafa na vikosi vyote vinaendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo ili kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Hata hivyo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mito na Mifereji kwakuwa ndio chanzo Cha mitaro kuziba na kusababisha Mafuriko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...