Na Mwandishi wetu, Manyara
MKUU
wa Takukuru Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amezipongeza
Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Mji wa Babati, kwa
kutoa mikopo ya shilingi milioni 200 isiyo na riba kwa makundi maalumu.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Babati, Makungu amesema Halmashauri hizo
mbili kwa mwaka 2019/2020 zimetoa mkopo wa shilingi milioni 200 kwa
makundi maalumu ya wanawake, vijana na walemavu.
Amewahimiza
wananchi ili kupunguza kazi ya kushughulikia mikopo umiza wajiunge
kwenye vikundi ili kupata mikopo halali inayotolewa bila riba.
Amesema
kwa muda sasa wamekuwa wakishughulikia kurejesha fedha kwa wananchi
waliodhulumiwa kutokana na wakopeshaji wasio na leseni kinyume cha
sheria ya fedha The Microfinance Act, 2018.
Hata
hivyo, ameufahamisha umma kuwa TAKUKURU wanazo taarifa kuwa wapo baadhi
ya mawakala wa vyama vya kisiasa wanaochukua vitambulisho vya kupiga
kura kwa kuwadanganya kuwa watawapa mikopo.
Amesema
wanawake hao wanapaswa kufahamu kuwa kadi hizo zinakusanywa ili
kuwanyima wao haki ya kuchagua kwa njia ya kura viongozi wanaowataka
kinyume cha ibara ya (21) ya katiba ya Tanzania.
Amesema
kifungu cha 16 cha sheria hiyo kimepiga marufuku kwa mtu kufanya
biashara ya fedha au kutoza riba bila ya kuwa na leseni na
atakayedhibitika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka
miwili jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.
Amewaonya
baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa wanaokusanya kadi za kupiga kura
hasa za wanawake kwa udanganyifu kuwa watawapa mikopo.
Amesema
wanawake hao wanapaswa kufahamu kuwa kadi hizo zinakusanywa ili
kuwanyima wao haki ya kuchagua kwa njia ya kura viongozi wanaowataka
kinyume cha ibara ya (21) ya katiba ya Tanzania.
Amesema
kifungu cha 16 cha sheria hiyo kimepiga marufuku kwa mtu kufanya
biashara ya fedha au kutoza riba bila ya kuwa na leseni na
atakayedhibitika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka
miwili jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.
"Kwa
wale ambao kadi zao za kupigia kura zimechukuliwa na walaghai hao, pia
wale ambao kwa bahati mbaya wamepoteza kadi hizo ili kurejesha haki hiyo
ya kikatiba Tume ya uchaguzi imeshatoa utaratibu ambao kitambulisho cha
Taifa na leseni ya udereva itatumika," amesema Makungu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...