Yassir Simba, Michuzi TV

KAMPUNI ya Wasafi Media, kupitia vituo vyake vya Wasafi  leo Novemba 24, 2020 imezindua rasmi tamasha linalokwenda Kwa jina la Wasafi Tumewasha na Tigo, ambapo watangazaji, waandaaji wa vipindi pamoja na timu nzima ya Wasafi Media na wasanii, itafanya ziara maalumu ya kutembelea Mikoa mbalimbali ambako Wasafi Fm imezindua masafa yake na inasikika.

Akizungumza na wanahabari katika makao Mkuu ya Wasafi Media yaliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,  Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amesema kampeni ya Wasafi Tumewasha na Tigo ni ziara yanye lengo kuu la kusherekea kwa ukaribu pamoja  na wasikilizaji  na watazamaji wao mafanikio makubwa ambayo kampuni hiyo imeyapata tangu kuanzishwa Kwake takribani katika miaka miwili iliyopita huku wilaya ya Kahama iliyopo Mkoani Shinyanga ikabarikiwa kufungua ziara hiyo rasmi huku Mikoa kama Mbeya, Arusha, Dodoma, Mwanza pamoja na Dar es Salaam ikitarajiwa kufuatia hapo baadae. 

Aidha, Diamond Platnumz amedokeza kuwa ratiba za Wasafi Tumewasha na Tigo zitaanza asubuhi kwa kushiriki katika Michezo mbalimbali na baada ya Michezo ni burudani ya nguvu kutoka Kwa wasanii mbalimbali huku msanii Ray Vanny akiahidi kufanya onyesho kabambe na kukata kiu ya mashabiki ambapo onesho hilo halitakuwa na kiingilio.

Naye Mkuu wa Vipindi wa Wasafi Fm,  Nelson Kissanga amesema ziara hiyo ya Wasafi Tumewasha na Tigo ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa Watanzania kutokana na namna walivyoipokea radio yao huku akiambatanisha na takwimu ambazo zinadai Kwa sasa Wasafi Fm ndiyo radio inayoongoza  kwa kusikilizwa na idadi kubwa ya Watu kupitia vipindi vyao kama Sports Arena, Good Morning, Mashamsham pamoja na Mgahawani.

Naye Mtangazaji wa kipindi cha Good Morning, Zembwela ametumia hafla hiyo kumtambulisha Zungu kama mtangazaji mpya wa Wasafi Fm akitokea Clouds Plus huku pia akiahidi kuendelea na ufanisi wa hali ya juu katika kazi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...