Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akizungumza na viongozi wa michezo huku akiwataka kuhakikisha
kila mmoja anawajibika katika kutoa maoni, alipokuwa akifungua Warsha ya
kutoa maoni katika Rasimu ya Kanuni zitakazoasiliwa kwa ajili ya
kupinga mbinu haramu za matumizi ya madawa za kusisimua misuli na
kuongeza nguvu michezoni (Anti Doping) iliyofanyika Novemba 19, 2020
Jijini Dar es Salaam, (katikati) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Yusuph
Singo.Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Yusuph Singo akiwasihi Wadau wa Michezo
kulichukulia kwa uzito suala la Anti Doping na kuharakisha utoaji maoni,
ili kuepusha taifa kufungiwa ushiriki wa michezo ya Kimataifa, Novemba
19, 2020, Jijini Dar es Salaam, katika ufunguzi wa Warsha ya kutoa maoni
ya rasimu ya kanuni zitakazo asiliwa za kupinga mbinu haramu za
matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akisalimia na Mchezaji wa Kutunisha Misuli aliyewahi kuwa Mr.
Tanzania (1996&1997) Bw. Fike Wilson, mara baada ya ufunguzi wa
Warsha ya kutoa maoni ya Rasimu ya Kanuni zitakazoasiliwa za kupinga
mbinu haramu za matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu
michezoni iliyofanyika leo Novemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha
wazamani waliyoliletea taifa sifa kubwa katika mchezo wa riadha
Bw.Nyambui watatu kushoto na wa kwanza kulia ni Bw.Philbert Bayi, mara
baada ya ufunguzi wa wa warsha ya kutoa maoni ya Rasimu ya Kanuni
zitakazo asiliwa za kupinga mbinu haramu za matumizi ya dawa za
kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni iliyofanyika leo Novemba
19, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini, waliyohudhuria Warsha ya kutoa maoni ya Rasimu ya Kanuni zitakazoasiliwa za kupinga mbinu haramu za matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni iliyofanyika leo Novemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Michezo wakifuatilia Warsha ya kutoa maoni ya Rasimu ya Kanuni zitakazoasiliwa za kupinga mbinu haramu za matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni iliyofanyika leo Novemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam.
*******************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
19/11/2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo kuwa wabunifu na kuandaa mikakati ya kukuza na kuendeleza michezo nchini.
Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Warsha ya Wadau wa Michezo nchini ya kutoa maoni ya katika rasimu ya Kanuni za Taifa za Kupinga mbinu haramu na matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni (Anti Doping).
Akizungumza katika Warsha hiyo Katibu Mkuu huyo na Msemaji Mkuu wa Serikali alisisitiza kuwa kila kiongozi wa Chama na Mashirikisho ya Michezo atimize wajibu wake kwa kutoa maoni ili kujiepusha na kero ya wanamichezo kuja kufungiwa kushiriki michezo na kuliletea taifa aibu.
“Najua mnafahamu kuwa taasisi hii ya kupinga matumizi ya mbinu haramu na dawa za kuongeza nguvu michezoni namna ilivyo na nguvu hivyo ni vyema suala hili mkalifanya kwa umakini, ili kuiepusha nchi kuwekewa vikwazo vya kushiriki michezo mbalimbali kimataifa,” alisema Dkt.Abbasi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Michezo Tanzania Bw.Yusuph Singo alisema Kamati ya Anti Doping kwa sasa imefanya kazi ya kuandaa kanuni ambazo zitakazo asiliwa na kuwa za kitaifa na badae serikali itaunda sheria ya kusimamia masuala hayo ya kupinga mbinu haramu michezoni.
“Kenya walisitishiwa kushiriki mashindano ya Kimataifa kwa kukosa “codes” ambazo zinaendana na mazingira ya nchi yao, ambazo ndiyo hizi kanuni tulizoandaa hivyo, ningependa suala hili tulichulie uzito na tulikamilishe haraka ili kuepusha taifa na chagamoto kama hii na tungependa kanuni hizi zianze kutumika mapema mwakani,” alisema Bw.Singo.
Halikadhalika nae Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Philbert Bayi aliishukuru Serikali kwa kufanikisha kusainiwa kwa mkataba huo wa kupinga matumizi ya mbinu haramu michezoni mnamo mwaka 2017, kwani Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi chache zilizokuwa bado hazijasaini mkataba huo.
Pamoja na hayo Dkt. Abbasi aliwaeleza viongozi wa Vyama vya Michezo kuwa mwanzoni mwa mwezi Desemba amepanga kutembelea vyama mbalimbali vya michezo nchini, kwa lengo la kufahamu changamoto na mikakati ya kukuza michezo ambapo alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano inataka kuacha alama katika michezo hivyo watoe hoja za nini kifanyike ili kuendeleza michezo mbalimbali kwa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...