Mkurugenzi wa kitengo maalumu cha vilainishi wa Total Tanzania  Anam Mwemutsi, , akizungumza  na waandishi wa habari, katika ziara ya wateja wa Total waliotembelea kiwanda cha vilainishi cha Total kilichopo vetenari, Temeke kujionea uzalishaji wa vilainishi vya Total, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka  2020. Kushoto Meneja Biashara wa kiwanda hicho, Amri Khamis, na kulia ni Meneja Uendeshaji, Lameck Mose. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu  ni  “Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja, ni mshirika”. Leo jijini Dar es Salaam.



Wataalamu wakiwa wameambatana na wateja wa bidhaa mbalimbali wakiangalia namna uzalishaji wa bidhaa za Total zinavyozalishwa katika kiwanda cha kampuni hiyo ikiwa ni maadhimisho ya wiki kwa wateja kwa mwaka 2020, leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi na baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja  wakati ya maadhimisho ya wiki kwa wateja ambapo leo wateja wa bidhaa za Total walitembelea kiwanda cha Total kinachozalisha vilainishi vya magari, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Total mara baada ya kupata mafunzo na kutembelea kiwanda hicho na kuona namna bidhaa ikiwemo vilainishi zinavyozalishwa leo jijini Dar es Salaam.

Mafunzo yakiendelea.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPUNI ya mafuta ya Total, ambayo ndio kampuni inayoongoza katika sekta uuzaji na usambazaji wa mafuta na vilainishi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, wamehimizwa kutumia vilainishi vyenye ubora ili injini za magari yao zidumu kwa muda mrefu.

Wito huo, umetoleo leo na Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania  Jean-Francois Schoepp  wakati wa ziara maalum ya wateja wakubwa wa vilanishi vya magari vya Total, kutembelea kiwanda cha vilanishi cha Total, ili kujionea namna  vilainishi hivyo vinavyotengenezwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya Total, inayoendelea kwa wiki  hii.

Jean-Francois Schoepp, amesema, injini za magari zinachakaa upesi na kuchoka mapema, kutokana na madereva kutumia vilainishi vyenye ubora hafifu, na kuwashauri kutumia vilainishi  vyenye ubora wa juu kutoka Total, ambavyo hupunguza pia muda wa kufanya  marekebisho ya  mara kwa mara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo maalumu cha vilainishi wa Total, Anam Mwemutsi amesema kampuni hiyo imetenga wiki ya huduma kwa wateja ili kuona huduma wanazozipata pamoja na kubaini changamoto zao na kuzitatua.

Amesema kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikizingatia utoaji wa huduma kwa viwango vya kimataifa kwa wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa mwisho wa mafuta na bidhaa nyingine vikiwemo vilainishi.

Aidha ameeleza kuwa katika maadhimisho ya wiki ya wateja wafanyakazi hutembelea vituo vya kutolea huduma  na kuona namna wateja wanavyopata huduma na katika siku ya leo wateja wamepata fursa ya kutembelea kiwanda cha Total ambacho hutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vilainishi.

Mmoja ya wateja waliotembelea kiwanda hicho, Mhandisi. Honeywick Kalenge kutoka Tanga Cement amesema kuwa bidhaa za Total ni bora hasa katika mazingira ya Tanzania kwa kuwa watumiaji wa bidhaa hizo huepuka matengenezo ya mara kwa mara.

Total ni Kampuni ya nne kwa ukubwa duniani na ya kwanza kwa ukubwa barani Afrika na Tanzania ambako ina vituo vya mafuta vipatavyo mia moja, kiwanda cha kuzalisha vilainishi  na ipo mbioni kutekeleza mradi wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka Tanzania hadi Uganda na wanasherekea zaidi ya miaka 50 nchini Tanzania kwa mafanikio lukuki ikiwemo kuwafikia wateja wengi zaidi na kutoa huduma bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...