WAUZAJI na wasambazaji wa mbao wametakiwa kuwasiliana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) ili waweze kuelekezwa ni viwango gani vinafaa kutumika kwenye bidhaa zipi za mbao na ni namna gani wanaweza kuzalisha ili waweze kuendana na matakwa ya viwango vya ubora.

Akizungumza na Mwandishi wetu Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango katika sekta ya Ujenzi na Majengo kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) Mhandisi Kakuru Chiganga amesema viwango vya ubora katika mbao vinakuwa vinaelezea muonekano wa nje ambao unaweza kukubarika na unakidhi ubora wa kimataifa.

"Mbao hizi tunapozitumia kuna muonekano ambao unakubarika maana kuna mbao zinatumika katika kutengeneza Furniture lakini kuna mbao zinatumika kwenye shughuli nyingine kwa mfano mirunda, kuezeka au kutengeneza fremu za madirisha na milango". Amesema Mhandisi Chiganga.

Aidha Mhandisi Chiganga amesema miongoni mwa matakwa mengine kwenye viwango vya ubora wa mbao ni uimara wa ubao wenyewe na bidhaa zinazotokana na mbao.

"Kuna matakwa ambayo yamekuwa yamewekwa kwaajili ya kuelezea uimara wa ubao na sehemu ambayo inaweza kutumika". Amesema Mhandisi Chiganga.

Sehemu nyingine ambayo imekuwa ikielezewa kwenye viwango vya ubora wa mbao ni uimara wa kupambana na unyevunyevu ambapo unaelezea kwamba ubao unatakiwa kuwa na unyevunyevu kiasi gani ili uweze kutumika sehemu na kudumu kwa muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...