

*******************************************
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Simbachawene akiiwakilisha Tanzania katika Mkutano Maalumu wa Nane wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) uliofanyika leo Desemba 4, 2020 kwa njia ya mtandao katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Katika Mkutano huo uliohudhuriwa pia na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, viongozi hao kutoka barani Afrika wamejadili masuala muhimu na agenda za Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA-5) utakaofanyika Februari, 2021 na kukubaliana msimamo wa pamoja wa Afrika katika kushiriki Mkutano huo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...