Ili kuendeleza dhamira yao ya kuwa kinara kwa kadi za malipo, benki ya BancABC Tanzania leo imetangaza kuzindua Kubwa Lao kwakufanya maboresho ya kiteknolojia Kidigitali yatakayowafaidisha wateja wote nchini kufurahia huduma zaidi wanapofanya malipo kwa kutumia kadi zao ambapo sasa wameongeza teknolojia ya 3D yenye ulinzi zaidi wakati wa kutumia kadi kila unakapofanya manunuzi kupitia mtandao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa wateja wadogo wadogo na wakubwa BancABC Tanzania Joyce Malai alisema Sasa usalama zaidi umeongezwa kupitia teknolojia mpya hii ambayo inaweka ulinzi zaidi kwa kuzuia mtu ambae si mmiliki wa kadi ya visa ya BancABC kuitumia kwa kufanya manunuzi mtandaoni bila ridhaa ya mmiliki. Hii ni kwa sababu teknolojia hii ya kisasa inatusaidia kumjua mtumiji halali na hivyo kuzuia udukuzi/wizi wa kimtandao.
Baada ya hivi karibuni kuzindua kadi ya Visa ya malipo ambayo inamfanya mteja kufanya malipo kwa njia ya mtandao kwa uhuru Zaidi, kwa kadi za BancABC ambazo zimeongezewa teknolojia mpya ya 3D kuipa huduma itaendelea kuifanya BancABC Tanzania kuwa kinara kwenye matumizi ya kadi ya Visa na kuwafanya wateja kuendelea kufurahia huduma ambazo ni salama Zaidi, rahisi na za haraka kwa kufanya malipo kwa njia ya mtandao na hata katika mashine za POS.(yaani mashine za malipo mbalimbali)
“Ikiwa BancABC Tanzania ndio benki ya kwanza kuzindua kadi hizi za malipo ya kabla, lengo letu ni kuendelea kuongoza kwenye soko kwa kuleta kadi zenye ubunifu wa hali ya juu ili kuwafanya wateja wetu kuendelea kufarahia huduma salama, rahisi na ambazo hazina kupoteza muda kwa kufanya malipo kwa njia ya mtandao”. Alisema Malai
Malai aliongeza kuwa wakati unapofanya manunuzi yako ya kitu chochote mtandaoni iwe kwa kompyuta au kifaa chochote cha kidijitili,programu hii iliyoongezwa itakuongoza kwa ufanisi zaidi kuhakiki taarifa zako ili kuthibitisha utambulisho wako. Hii itasaidia kuhakiki taarifa zako na kukulinda na wadukuzi/ wezi wa mitandao.
Mkuu wa Kitengo cha Kiditali BancABC Lameck Mushi alisema kuwa BancABC imeshinda tuzo tatu ya Visa maarufu kama “Visa E-commerce Issuing Growth Award” kutokana na huduma zake za kipekee za malipo ya mtandaoni ambazo ni salama na nafuu hapa nchini. Benki hiyo imejishindia tuzo hiyo ya Visa kutokana na matumizi ya kadi zake za Visa ambazo wateja wanatumia kulipia huduma mbali mbali kwa njia ya mtandao.
Mushi aliongeza kuwa kadi za malipo ya kabla za fedha za Tanzania zimeunganisha na Applikesheni ya Mobi ambayo inamfanya mteja kuweza kuweka au kutoa pesa kwenye akaunti kwa kutumia simu ya Mkononi. Kwa sasa, hakuna sababu ya kutembelea tawi lolote la benki kwa ajili ya kufanya muamala wa aina yoyote.Pia mteja anaweza kupata salio la akaunti yake, taarifa za miamala yake akiwa mahali popote na atapokea ujumbe mfupi wa maneno kwa kila muamala unaofanyika.
Hakuna haja ya kuhangaika wapi unaweza kutumia kadi za Visa kwani huduma zake zinapatikana masaa 24 kwa siku saba za wiki kwenye ATM za Visa milioni 2.7 duniani kote na kwenye maduka milioni 46 ya rejareja ulimwenguni kote huku kwa Tanzania ikipatikana kwenye mashine 400 za ATM za Visa na maduka Zaidi ya 1000 yanayokubali kadi ya Visa” alisema Mushi huku akiongeza kuwa kadi ya 3D Visa inakuja na ikiwa na huduma kwa fedha za TZS, Dola, Paundi, Randi, Euro na Yarn.
Mkuu wa Kitengo cha huduma za kidigitali wa BancABC Tanzania (kati kati) akiongea mwishoni mwa wiki wakati wa kutangaza kuzindua Kubwa Lao kwakufanya maboresho ya kiteknolojia Kidigitali yatakayowafaidisha wateja wote nchini kufurahia huduma zaidi wanapofanya malipo kwa kutumia kadi zao ambapo sasa wameongeza teknolojia ya 3D yenye ulinzi zaidi wakati wa kutumia kadi kila unakapofanya manunuzi kupitia mtandao. Kulia ni Mkurugenzi wa wateja wadogo wadogo na wakubwa BancABC Tanzania Joyce Malai na Kushoto ni Mkuu wa Uhudma za Uwakala benki hiyo Mwita Rhoba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...