CHUO chaTaifa cha Usafirishaji (NIT), kimeaswa kuendelea kuwa wabunifu  na kufanyakazi kwa bidii ili kufanya Chuo hicho kuwa mahali salama na sahihi pa kujifunza katika kuendeleza sekta ya Uchukuzi.

Amesema katika kuhakikisha nchi inaendelee kukua kiuchumi ubunifu ni jambo la muhimu, hivyo ninawashauri walimu na wataalamu mbalimbali nchini kuhakikisha wanawaanda wanafunzi kuwa wabunifu ili pia kuwa tayari kukabiliana na soko la ajira


Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa Mahafali ya 36 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo mwaka huu wa 2020 jumla ya wahitimu 1,738 wametunukiwa tuzo kwa kozi mbalimbali.

Amesema, Serikali  umeweka nguvu kubwa kuhakikisha sekta ya uchukuzi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, Reli, meli na mnunuzi wa ndege, lakini hayo yote hayatokuwa na maana kama nchi itaendelea kumtegemea wataalamu kutoka nje

Aidha, Kasekenya amewataka wanafunzi hasa wa vyuo vikuu nchini kuwa wabunifu na kusoma kwa bidii ili pindi  wanapomaliza vyuo waweze kuwa na ujuzi wa kutosha utakaowasaidia kujiajiri.

Aidha Kasekenya amewashauri wahitimu hao kutoridhika na utaalamu wa waliopata vyup oni tu bali waendelee kutafuta utaalamu wa juu zaidi ili Taifa liwe na wataalamu wa kutosha na we wenye sifa zote zinazohitajika kwenye sekta ya uchukuzi.

"Ni ninawaasa wanafunzi mnaoendela na masomo kuwa wabunifu na kusoma kwa bidii ili mmalizapo masomo M yenu muweza kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha maana ili iwe rahisi kwenu kujiajiri hasa ukizingatia kuwa uchumi wa viwanda inahitaji nguvu kazi yenye maarifa na ujuzi zaidi.

"Kuhitimu kwenu kuwe mwanzo wa safari nyingine kitaaluma, hakikisheni mnajiendeleza kielimu," alisema
Pia Kasekenya ameipongeza NIT kwa kuanza kutoa mafunzo ya usafiri wa a maji pamoja na kuongeza wigo kwa mafunzo ya Reli kitu ambacho kitaipunguzia serikali mzigo wa kugharamia Mafunzo hayo nje ya nchi ambayo hutolewa kwa garama kubwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo  cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema, idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika chuo hicho imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo kusababisha ongezeko la wataalamu katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji.

Amesema katika kipindi cha miaka saba idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa asilimia 258, kutoka 3248 mwaka 2014/2015 hadi wa wanafunzi 11,640 kwa mwaka 2019/2020 huku idadi ya wataalamu ikiwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Chuo.


"Chuo kinalazimika kutumia fedha nyingi kuwalipa wahadhiri wa muda ili kuziba upungufu wa wataalamu ili kuendelea kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa, amesema Profesa Mganilwa

Aidha alisema katika kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa wataalam mbalimbali chuo hicho kimeanzisha kituo cha umahiri cha mafunzo ya taaluma za anga na operesheni za usafirishaji kwa mikopo kutoka Benki ya Dunia.

"Fedha hizi za mkopo zitatumika kujenga madarasa, maabara, katakana pamoja na kununua vifaa vya mafunzo ikiwemo mock up na ndege kwa ajili ya mafunzo ya urubani," alisema

Profesa Mganilwa amesema, katika kukabiliana na changamoto katika sekta ya usafiri wa majini kama uhaba mkubwa wa rasilimali watu na uchakavu wa miundombinu chuo kimeendelea kutoa mafunzo katika ngazi za stashahada, shahada na stashahada ya Uzamili, kuandaa mitaala ya programu za usafiri kwa njia ya maji na Mafunzo ya kazi fupi fupi.


Pia amewapongeza wahitimu wote kwani juhudi na uvumilivu wao ndiyo nguzo ambazo zimewafikisha katika kilele cha mafanikio hayo na kwamba sasa mafanikio yao hatapimwa tena kwa mitihani bali kwa kuangalia vy viwango vya ufanisi katika utendaji kazi wao.

"Mafanikio yenu hayatapimwa kwa mitihani tena bali mtapimwa kwa kuangalia viwango na ufanisi katika utendaji wa kazi zenu.hivyo mkatimize majukumu yenu kwa ufasaha kwa kujituma, ubunifu, nidhamu na uadilifu wa hali ya juu.

Baadhi ya wahitimu kozi mbali mbali wa Chuo cha NIT wakifurahia wakati wa mahafali ya 36 yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki
Viongozi wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT, wakiwa katika mahafali ya 36 ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo NIT Profesa Zacharia Mganilwa kulia, akisoma hotuba wa wakati wa mahafali ya 36 ya Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam, katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Msongwe Kasenyeka  na kushoto ni Mwenyekiti wa baraza la uongozi chuoni hapo, Mhandisi Blasius Bavo Nyichomba.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Msongee Kasekenya (katikati) akiwa katika maandamano wakati wa mahafali ga 36 ya Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo NIT Profesa Zacharia Mganilwa na kushoto ni Mwenyekiti wa baraza la uongozi chuoni hapo, Mhandisi Blasius Bavo Nyichomba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...