Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akihutubia Wahitimu wa  katika Chuo cha Uadishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) kwenye  mahafali yaliyofanyika  Desemba 18,2020 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwatunuku  vyeti wahitimu wa Astashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) kwenye mahafali yaliyofanyika  Desemba 18,2020 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uadishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) wakiwa kwenye mahafali yaliyofanyika Desemba 18, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Chuo cha Uadishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) Bw.Johson Swoa akizungumza kwenye  mahafali  ya wahitimu wa Astashahada na Stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yaliyofanyika  Desemba 18,2020 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Astashahada na Stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) pamoja viongozi wa Chuo hicho kwenye mahafali yaliyofanyika Desemba 18, 2020 Jijini Dar es Salaam.

*****************************************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Katibu  Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ameviagiza Vyombo vyote vya Habari nchini kutoa nafasi kwa wahitimu wa taaluma ya Habari kufanya  mazozezi  kwa vitendo katika vyombo hivyo  ili waweze kujendeleza  katika taaluma hiyo.

Dkt Abbasi ametoa agizo hilo Desemba 18,2020 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa Astashada na Stashada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambapo amesema kuwa lengo la kutoa nafasi kwa wahitimu hao ni kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri katika taaluma hiyo.

“Tutahakikisha kwenye kuhuisha leseni ya chombo cha habari pamoja na mambo mengine, sifa nyingine lazima uonyeshe uthibitisho wa kuchukua wanafunzi wangapi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika chombo chako” alisema Dkt.Abbasi

Huku akisistiza kuwa hapa nchini kuna  idadi ya Magazeti na Majarida zaidi ya 230, Redio 185 zinazotangaza katika ngazi ya Mikoa, kitaifa na kimataifa, pamoja na runinga  takriban 40 ambazo zimesajiliwa nchini na kupewa leseni  hivyo ni lazima kila chombo kutoa nafasi kwa wanachuo wa taaluma  hiyo kufanya mazoezi kwa vitendo  ili taaluma hiyo izalishe wataalamu wengi zaidi.

 Vilevile Dkt. Abbasi amwaeleza wahitimu hao baadhi ya siri za mafanikio ikiwemo Kuweka malengo, kuweka malengo makubwa pamoja na kuwa na malengo yanayotekelezeka.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Bw. Johson Swoa amewapongeza wanafunzi hao kwa kuhutimu na kutuunikwa vyeti ambapo ameeleza kuwa chuo hicho kimefanikiwa kuzalisha wataalamu wengi ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya habari ikiwemo kutangaza, kuandika na kuhariri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...