
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya Wakurugenzi na Mameneja wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi nchini kupitia Chama chao cha TAMASCA kuendelea kutunza heshima ya makampuni hayo na kufuata misingi ya vibali vinavyowaongoza ikiwa ni pamoja na sheria za nchi.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa siku moja wa Chama cha Makampuni ya Ulinzi Watu Tanzania TAMASCA uliofanyika jijini Dodoma, wenye lengo la kufanya tathimini na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.
Akisoma risala mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Bwana Shawiniaufoo
Kimuto, amesema kuwa, licha ya Makampuni
binafsi ya ulinzi kuendelea kufanyakazi kwa uzalendo lakini bado wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo ikiwemo mafunzo ya weledi na umilikishwaji wa
silaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...