MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi limeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kudhibiti vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha za moto huku akitaja mafanikio hayo yametokana na jitihada na weledi wa askari wa Jeshi hilo pamoja na ushirikiano kutoka kwa wananchi.
IGP Sirro amesema hayo leo Mkoani Geita wakati alipofanya ziara ya ukaguzi ambapo amekutana na makamanda wa mikoa mitatu ya Geita, Kagera na Kigoma na kufanya tathimini ya mafanikio yaliyotokana na juhudi za kudhibiti matukio ya uhalifu.
Aidha, IGP Sirro pia amekutana na askari wa kikosi maalium cha kuzuia uhalifu ambapo askari hao walimuonyesha Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi silaha kadhaa za moto walizozikamata ikiwemo bunduki zilizotengenezwa kienyeji na kutumika kwenye matukio ya uhalifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...