Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo Dkt. Honest Kessy akuhutubia Washiriki wa mkutano wa kupitia Mpango Kazi wa Kutekeleza Kazi zinazohusu Lishe katika Sekta ya Kilimo  leo tarehe 22 Desemba, 2020 katika hoteli ya Nashera, Jijini Dodoma


MKURUGENZI wa Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo Dkt. Honest Kessy amesema Serikali imefanya juhudi kubwa ili kuhakikisha Sekta ya Kilimo mazao imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la utapiamlo aina ya udumavu; Ambapo udumavu umepungua kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi asilimia 32 mwaka 2018 na kuongeza kuwa ukondefu umepungua kutoka asilimi 3.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.5 mwaka 2018 ambayo ni chini ya kiwango cha malengo ya Shirika la Afya Duniani (WHA) cha asilimia 5.

 

Dkt. Kessy amesema licha ya juhudi hizo bado kuna haja kwa Wadau wote kwa kushirikiana na Serikali kuendelea kupunguza kiwango cha utapiamlo kwa kuwa inawezekana na kuongeza kuwa juhudi zinapaswa kulenga katika kuongeza uelewa, kuelimisha watu kuhusu tamaduni na kuongeza uelewa namna nzuri ya kubadili maisha ya watu kila siku kuhusu ulaji wa vyakula vya makundi yote.

 

Katika hotuba yake kwa Washiriki wa mkutano wa kupitia andiko la Mpango Kazi wa Kutekeleza Kazi zinazohusu Masuala ya Lishe katika Sekta ya Kilimo Dkt.Kessy amesema kulingana na taarifa ya matokeo ya mapitio ya nusu mwaka ya Mpango wa Kitaifa wa Lishe (Mid Term Review – MTR) ambayo ilifanyika mwaka 2019; Imeonyesha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula hususan zao la mahindi umekuwa ukiongezeka kutokana na msukumo mkubwa uliowekwa na Serikali lakini uzalishaji wa mazao mchanganyiko na ulaji usiofaa ili kukidhi mahitaji ya mwili umeonekana kutofanya vizuri ambapo kumekuwapo na kiwango cha juu cha udumavu.

 

Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula ameongeza kuwa mikoa inayoongoza kwa kuzalisha zao la mahindi imekuwa na changamoto kubwa ya udumavu. 

 

Mikoa hiyo ni kama ifuatavyo: - Njombe (Kiwango cha udumavu ni asilimi 53.6); Rukwa (Kiwango cha udumavu ni asilimia 47.9); Iringa (Kiwango cha udumavu ni asilimia 47.1); Songwe (Kiwango cha udumavu ni asilimia 43.3); Ruvuma (Kiwango cha udumavu ni asilimia 41) na mwisho ni mkoa wa Kigoma (Kiwango cha udumavu ni asilimi 42.3).Dkt, Kessy ameongeza kuwa tatizo la udumavu likishatokea halina tiba kwa sababu hiyo kuna haja ya kuunganisha juhudi kwa Wadau wengi kupambana na halio hii.

 

“Niseme kuwa udumavu hauna tiba, mfano udumavu ukimpata Mtoto mdogo, hali hiyo inaathiri maisha yake yote pamoja na makuzi na afya ya ubongo wake. Mtoto kama huyo hata darasani hawezi kuelewa katika masomo yake”. Amekaririwa Dkt. Kessy.

 

Wizara ya Kilimo ni miongoni mwa Wizara zinatotekeleza Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (National Multi- sectoral Nutrition Action Plan) uklioznza kutekelezwa mwaka 2016 na unataraji kuisha mwaka mwaka 2021. Vivyo hivyo Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili yaani ASDP II ambapo mikakati hii yote imetambua na umuhimu wa kilimo katika kuboresha lishe.

Dkt. Kessy amemaliza kwa kuwasisitiza Washiriki kutoa michango mizuri ambayo italenga katika kuboresha katika Mpango Kazi wa miaka mitano wa Kutekeleza Kazi zinazohusu Lishe katika Sekta ya Kilimo hususan masuala ya lishe ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu kwa Watanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...