NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
HALMASHAURI ya Mji Kibaha ,mkoani Pwani, inatarajia kukusanya kiasi cha sh.bilioni 3.9 ya mapato kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Katibu
tawala wilaya ya Kibaha Sozi Ngate ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa
kuapishwa madiwani wa Halmashauri ya mji huo, alisema makusanyo ya
mwaka 2019/2020 ni bilioni 3.2 ambapo kwa sasa imefikia asilimia 86.
Kwa hatua hiyo ,alieleza ili kufikia malengo ,Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani wanapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato.
"Kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali tunapaswa kuhakikisha tunakusanya
mapato kupitia vyanzo vyetu mbalimbali ambapo makusanyo ya mwaka
2019/2020 ni bilioni 3.2 ambapo kwa sasa imefikia asilimia 86," alisema
Ngate.
Alibainisha,
makusanyo ndiyo uti wa mgongo wa Halmashauri hivyo lazima madiwani
wahakikishe wanasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato.
Aidha
alisema kuwa ili kuleta mafanikio lazima kila mmoja awajibike kwenye
nafasi yake na kubwa ni katika kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba
alieleza, watazingatia njia za ukusanyaji ili kufikia malengo
yaliyowekwa ya ukusanyaji na watahakikisha fedha za miradi ya maendeleo
zinatumika kutokana na thamani yà fedha (Value for Money).
Nae
makamu mwenyekiti wa Halmashauri Selina Wilson alisema watahakikisha
wanawaletea maendeleo wananchi,kusimamia ujenzi wa miundombinu na
kufanya utatuzi wa migogoro mbalimbali ili wananchi waishi kwa amani.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Mji Kibaha Jenifa Omolo alifafanua, Halmashauri
itahakikisha inahudumia wananchi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa
kutumia mapato yanayokusanywa.
Madiwani walioapishwa ni 21 wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo 14 ni kutoka kwenye kata na watano ni wa viti maalum.
Awali
kwenye uchaguzi wa mwenyekiti Musa Ndomba alichaguliwa kuwa mwenyekiti
wa Halmashauri kwa kupata kura 21 na makamu mwenyekiti Selina Wilson
alipata kura 21.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...