RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.
Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati hiyo iliofanyika katika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar leo 8/12/2020.(Picha na Ikulu)
………………………………………..
Makamo wa kwanza wa Rais mteule Maalim Seif Sharif Hamad
aliyeapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk Hussein Ali Mwinyi ametakiwa kufanya kazi kwa dhati na kukiheshimu
kiti cha Rais.
Ikiwa kiongozi huyo
ameingia kwenye suk kwa lengo la kushindana na Rais ili aje kumtoa
madarakani katika Uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025 maelewano tarajiwa
yatapwaya.
Ushauri huo
umetolewa Balozi Mstaafu Ali Abeid Karume mara baada ya Rais wa
Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kumuapisha huko ikulu na kuwa rasmi
Makamo wake wa kwanza wa Rais.
Balozi Karume
amesema licha ya Maalim Seif ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu,
anapaswa kukiheshimu kiti cha Rais kwani Dk Mwinyi ndiye mwenye urais.
Ameitaja kazi ya
Maalim Seif kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ni kumshauri
Rais na kutekeleza majukumu yote atakayopangiwa na Rais.
Balozi Karume
amesema ukongwe wa Maalim Seif katika medani za siasa na utawala kisiwe
kigezo cha kumfanya adhani yuko sawa na Rais au Rais atapokea maelekezo
kutoka kwake.
Amesema badala yake kazi alionayo ni ya ushauri kwa Rais hivyo Rais atakuwa na hiari ya kukubali ushauri huo au kuukataa.
Aidha Balozi amsema
ikiwa kiongozi huyo wa upinzani kwa dhati yake aheshimu matakwa ya Rais
kisera, kimalengo na kimajukumu anaamini kazi ya kujenga nchi
itafanyika kwa umakini.
Mtoto huyo wa pili
wa Rais wa Kwanza Zanzibar hayati Mzee Abeid Amanj Karume ,amesema kila
mwanasiasa ajue urais haupatikani kwa njama au kwa mizengwe.
Badala yake amesema urais humfika yeyote kwa kudra, bahati na uweza wa mungu wala si kwa hujuma au kwa makeke.
Mwadiplomasia huyo
amekitaja chanzo cha mvutano katika suk awamu ya saba amedai kulikuwa
na hali ya kutoelewana kati ya Rais na Makamo wake wa kwanza wa Rais.
Amesema jambo la kusikitisha baadhi ya siri za SMZ zikizagaa mitaani kabla hata ya vikao vya BLM havijamalizika Ikulu.
Amemtaja Maalim
Seif kuwa ndiye aliyeanza kumtupia vijembe Rais kwenye mikutano ya
hadhara , Rais alipoona mambo yanazidi akamjibu na hapo ndio ufa
ulipojitokeza.
Amesema hadi
wanakwenda katika Uchaguzi mwaka 2015 maelewano yao yalishatetereka
hivyo akasema hategemei kama hali hiyo itajirudia tena.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...