Na
Mary Gwera, Mahakama
MSAJILI wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari ‘IRMCT’, Bw.
Abubacarr Tambadou ameahidi kuendeleza ushirikiano wa utendaji kazi baina ya
Mahakama hiyo na Mahakama ya Tanzania.
Akizungumza
wakati alimpotembelea Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini
kwake leo Desemba 02, 2020, Msajili huyo alisema kuwa yupo tayari kuendeleza
kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na ‘IRMCT’ kwa maslahi ya
Taifa.
“Nina furaha kukubali ombi langu la kuonana na
wewe licha ya kuwa na majukumu mengi ya kazi, lengo la mimi kuja kukutembelea
ni kujitambulisha rasmi na kuomba kuendeleza ushirikiano wa kikazi baina yetu,”
alieleza Bw. Tambadou.
Vilevile,
Bw. Tambadou alieleza kuwa Mahakama ya Tanzania itumie vyema uwepo wa Mahakama
ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari ‘IRMCT’ kama tija ya kujua
zaidi sheria za kimataifa.
Naye,
Mhe. Jaji Mkuu alimuahidi Msajili huyo kutoa ushirikiano zaidi na kuahidi
kumtembelea pindi atakapokuwa Arusha.
Aidha;
Mhe. Jaji Mkuu alipataa wasaa wa kumueleza Msajili huyo kuwa Mahakama ipo
katika maboresho mbalimbali yanayolenga kurahisisha na kusogeza huduma za haki
karibu zaidi na wananchi.
Hali
kadhalika Mhe. Jaji Prof. Juma alimueleza Bw. Tambadou kuwa Mahakama ya
Tanzania kwa sasa ipo katika maandalizi ya kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa
kwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Bw.
Abubacarr Tambadou alichaguliwa kuwa Msajili wa Mahakama hiyo Julai mosi mwaka
huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...