Na Munir Shemweta, SIHA
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema sheria
inaruhusu kuandikwa majina yote mawili ya wenza katika hati za umiliki
ardhi.
Lukuvi alisema
hayo tarehe 19 Desemba 2020 wilayani Siha mkoa wa Kilimanjaro
alipokwenda kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Watawa wa Shirika la
Kanisa Katoliki na wananchi wa kitongoji cha Mlangoni kuhusu Shamba la
Kirari.
Alisema, Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa ikisajili Hati nyingi
zenye majina yote mawili ya wenza na wengine husajili na majina ya
watoto wao.
Kwa mujibu wa
Lukuvi, siyo kweli kwamba Hati lazima isajiliwe kwa jina moja tu la mke
au mume bali wote wawili wanaruhusiwa kitu cha msingi wawe na sifa za
kumilikishwa.
Lukuvi
alisema, hiyo ni fursa kwa wanawake kushawishi waume zao katika
kutekeleza suala hilo kwa kuwa sheria iko wazi na hakuna Afisa Ardhi
atakaye hoji suala hilo.
"Akina mama mna ushawishi mkubwa washawishini waume zenu waandike majina mawili ili kuepuka mgogoro" alisema Lukuvi
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, hata
mtoto chini ya miaka 18 anaweza kusajiliwa katika hati kwa masharti
kuandikwa pia jina la msimamizi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...