
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, akifungua mkutano wa kwanza wa mwaka 2020\2021 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) jijini Dodoma.
Baadhi ya uongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga, katika mkutano wao wa kwanza wa mwaka 2020/2021 uliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano wao wa kwanza wa mwaka 2020/2021 wa baraza hilo, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Wizara hiyo na uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), baada ya ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo.
***************************************
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa Majengo ya Serikali 85 nchi nzima yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 142 ikiwamo miradi ya “Buni – Jenga”.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, ameyasema hayo jjini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa 2020/2021 wa Baraza la Wafanyakazi wa wakala huo na kusisitiza kuwa hiyo ni hatua kubwa kitaasisi lakini hatua hiyo haijawaondoa moja kwa moja kwenye changamoto za kuchelewa kwa baadhi ya miradi ya ujenzi.
Mwakalinga ameutaka uongozi wa wakala kutazama kwa undani hatua gani walizofikia katika utekelezaji wa majukumu yao hususani namna wanavyoweza kushughulikia changamoto katika kila eneo la kiutendaji.
“Hakikisheni mnajitathimini kwa kina bado kuna changamoto za kuzifanyia kazi na Serikali yenu inawaamini katika utoaji ushauri na usimamizi wa miradi ya ujenzi na usimamizi wa miliki za Serikali”, amesema Katibu Mkuu huyo.
Aidha, ameupongeza Wakala kwa hatua nzuri waliyofikia katika miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwamo ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Saalam ambapo hapo awali kulikuwa na malalamiko mengi.
Mwakalinga ameitaka TBA kuendelea kujali masuala ya wafanyakazi kutoka sekta binafsi kwa kuzingatia kuajiri watu wengi kwenye miradi ya ujenzi hususani walinzi, babalishe, mamalishe, watalaamu wa ujenzi, mafundi, vibarua na wanafunzi wa taaluma zote kutoka vyuo vikuu ili kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na kupunguza umaskini nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala huo, Arch. Daud Kondoro, amemueleza Mgeni rasmi kuwa katika mkutano huo wajumbe wa baraza la wafanyakazi watapewa elimu ya “haki za mtumishi mahali pa kazi na wajibu wa mtumishi kwa mwajiri” ili iweze kuwasadia kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...