WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ndicho chombo muhimu na chenye mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

 

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Desemba 22, 2020) alipokutana na Bodi mpya ya taasisi hiyo katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

 

“Sisi Serikali tunapofurahi na kuwaambia Watanzania kwamba nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hatuachi kuzungumzia namna ambavyo sekta binafsi ilivyoshiriki kiiamilifu kuleta mabadiliko.”

 

Kikao hicho ambacho ni uetekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipozindua Bunge la 12, jijini Dodoma, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na TPSF.

 

“Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hii na kwenye changamoto tutahakikisha tunazipatia ufumbuzi kwa pamoja. Serikali inaimani kubwa na Taasisi hii ya Sekta Binafsi Tanzania.”

 

Kwa upande wao viongozi wa taasisi hiyo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa ushirikiano inaowapatia ambao unawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

 

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara Geofrey Mwambe na watendaji wa taasisi za Serikali wanaohusika na usimamizi na uratibu wa maendeleo ya sekta binafsi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...