*Profesa Mgaya ataja uimara wa Taasisi katika kufanya utafiti katika sekta ya afya.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
TAFITI zinazofanyika nchini hasa zilizo afya zinatakiwa kudhibitiwa na zisiweze kutumika na watu wengine ikiwa ni kuweka mifumo ya uhifadhi wa tafiti hizo.
Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge wakati akizindua Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) yaliyofanyika katika Kituo Cha Mabibo Dar es Salaam na kuambatana na maonesho ya tafiti na Dawa na huduma za upimaji wa afya bure.
Amesema kuwa NIMR imefanya kazi kubwa katika mapambano ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona ikiwa kufanyia utafiti wa dawa ambayo wengi wanaitumia na inatoka mazingira yetu.
Kunenge amesema kuwa serikali imefanya mambo makubwa katika uimarisha wa Taasisi hiyo ambayo imekuwa imara pamoja na kuwa na watu wenye weledi ya kufanya kazi.
Aidha amewataka wananchi hasa wanaume kupima tezi dume katika hatua ya awali ya kupima damu na kujua kuwepo au kutokuwepo.
Hata hivyo amesema kuwa dawa ya 'NIMR Cough' amekuwa anaitumia na dawa hiyo imetengenezwa na mazao ya ndani na haina kemikali zilizotumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa. Yunus Mgaya amesema katika kuadhimisha miaka 40 wamepitia mambo mbalimbali lakini bado wamekuwa imara katika kuimarisha tafiti za magonjwa ya Binadamu.
Amesema moja ya majukumu ni kutoa kibali cha kufanya utafiti za afya pamoja na kufatilia matokeo ya tafiti hizo.
Amesema kuwa wanavituo nane katika Kanda ambavyo kila kituo kilianzishwa kwa makusudi yake ambavyo hadi sasa viko imara katika Utafiti wa Magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyoambukiza.
Profesa Mgaya amesema katika Maadhimisho hayo wananchi wameweza kutoa huduma za afya ikiwemo uchangiaji damu.
Pia Mkuu wa Kituo cha NIMR Muhimbili Profesa Sayoki Mfinanga amesema mafanikio ya mkakati Kituo kimeongeza uwezo wa kufanya tafiti kubwa za kitaifa na kimataifa toka tafiti tatu(3) kwa mwaka mwanzoni mwa mwaka 2000 hadi kufikia 35kwa mwaka 2020.
Amesema wamefanya utafiti wa dawa ya homa ya Uti wa Mgongo inayosababishwa na fangasi kwa waathirika wa Virusi vya Ukimwi na Ugonjwa unaochangia vifo kwa asilimia 25 ya vifo vya waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi ambapo baada ya utafiti na kufanya Tathimini wamepunguza vifo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...