Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia Wadau wa zao la chikichi katika mkutano aliouhitisha na kuuongoza kama Mwenyekiti katika ukumbi wa NSSF Mjini Kigoma leo tarehe 19 Desemba, 2020.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia Wadau wa zao la chikichi katika ukumbi wa NSSF Mjini Kigoma wengine kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Amandus Mzava, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias Kwandikwa pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda

Kaimu RAS mkoa wa Kigoma Bwana Vedastus Makota, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, Mkurugenzi Mkuu Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Japhet Justine wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika ukumbi wa NSSF Mjini Kigoma leo tarehe 19 Desemba, 2020.

Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt.Benson Ndiege akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge wakifuatilia hotuba ya hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika ukumbi wa NSSF Mjini Kigoma leo tarehe 19 Desemba, 2020.

***********************************

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 19 Desemba, 2020 amemuagiza Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda kuhakikisha anapeleka Maafisa Ugani katika Halmashauri sita zinazolima zao la chikichi mkoani Kigoma ili kuwaongezea maarifa Wakulima wa zao hilo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha Tanzania inaokoa zaidi ya bilioni 443 kutokana na kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

“Haiwezekani tukaendelea kutumia fedha hizo zote kwa kuagiza mafuta wakati tunaweza kulima na kuchaka mafuta ya mawese hapa hapa nchini; Naendelee kusisitiza, Serikali ya mkoa wa Kigoma iwe mfano kwa wengine”.

“Tija na uzalishaji wa zao la chikichi hapa Tanzania ipo chini ukilinganisha na nchi kama Malaysia ambayo uzalishaji wao umefikia tani 10 kwa hekta moja wakati sisi ni 1.6; Ndugu zangu lazima tupande miche bora kutoka kwa Taasisi zetu za Majeshi, TARI Kihinga na Sekta Binafsi ambao wamehamasika na kuotesha miche hiyo”.

“Nakumbuka miaka mitatu iliyopita, nilihamasisha Halmashauri sita za mkoa wa Kigoma kuanzisha vitalu vya miche bora pamoja na kuhamasisha Taasisi za Majeshi kama Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Jeshi la Magereza, Taasisi Binafsi kuanzisha vitalu ili mkakati wetu wa kuleta mapinduzi ya zao la chikiki, lifanikiwe kwa kuwa miti hii ya zamani; Tija yake ni ndogo”. Amekaririwa Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongeza kuwa,uzalishaji wa michikichi ya zamani ni tani 1.6 kwa hekta moja wakati miche bora uzalisha kuanzia tani 5 kwa hekta huku ikiendelea kuzalisha kwa zaidi ya miaka 20.

Pia, ameiagiza Wizara ya Viwanda na Wizara ya Kilimo kuhakikisha ziboreshe mazingira rafiki kwa Wakulima wa zao la michikichi nchini na uhakika wa soko.

“Naiagiza Wizara ya Viwanda na Wizara ya Kilimo kuhakikisha zinakuja na mkakati mzuri wa kuhakikisha Wakulima wa zao la chikichi pamoja na mazao yake;Wanapata masoko ya uhakika. Kaeni pamoja na mje na mkakati madhubuti kuhusu upatikanaji wa masoko kwa Wakulima wa zao la chikichi.” Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha,ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI) kwa kutekeleza agizo la kuanza kutoa mbegu bora ya zao la chikichi zaidi ya mbegu milioni 4.2 sambamba na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kuzalisha miche bora ya michikichi zaidi ya 456,252.

Awali, katika hotuba yake aliyoisoma leo katika ukumbi wa NSSF katika Halmashauri ya kigoma Ujiji,uliowashirikisha wadau wa zao hilo,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majalwa Majaliwa amesema hivi sasa mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni tani 570,000 kila mwaka wakati uwezo wa nchi kuzalisha ni tani 205,000 sawa na asilimia 36. Wakatihuohuo Serikali huagiza tani 365,000 sawa na asilimia 64 ya mafuta kutoka nje ya nchi; Ambapo Serikali hupoteza fedha kiasi cha shilingi Bilioni 443 kila mwaka.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, mazao yanayochangia upatikanaji wa mafuta ya kula nchini ni mazao ya chikichi, alizeti, karanga, pamba, ufuta na soya; ikumbukwe,  zao la chikichi ndio linaongoza kwa kutoa mafuta ya kula kuliko mazao mengine ya mafuta Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...