*Wananchi wajihadhari na mtandao batili unaotumia jina lake
WANANCHI wametakiwa kujihadhari na ujumbe unaosambazwa kwenye mtandao wa Facebook unaotumia jina la ‘Waziri Mkuu Kassim Majaliwa’ ukiwataka wajasiriamali watume pesa ili wapewe mkopo na taasisi iliyojitambulisha kama Kassim Majaliwa Foundation, kwani mtandao huo ni batili.
Ujumbe huo uonawataka wananchi watume namba za vitambulisho vya kupiga kura ili waweze kupatiwa mkopo anaotaka mkopaji ndani ya saa 24 kwa kutumia namba 0652 940 415. Namba hii imesajiliwa kwa jina la Yunus Milanzi.
Ofisi ya Waziri Mkuu inakanusha kuwepo kwa taasisi hiyo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa hana na wala hahusiki na Taasisi yoyote ya utoaji wa mikopo. Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia suala hili kwa karibu ili wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...