Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo (kulia) kufanya kazi usiku na mchana ili jengo hilo linaloendelea kujengwa liweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo lenye ghorofa nane lilitakiwa kukamilika Mwezi huu Disemba, 2020 lakini mpaka sasa limefikia asilimia 41. Wapili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati) akimsikiliza Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo alipokuwa anatoa maelezo ya mradi huo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi huo, leo. Simbachawene hajaridhishwa na ujenzi wa jengo hilo, hivyo amemtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kulikamilisha jengo hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Mradi Ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma, Martin Pallangyo (kushoto) kufanya kazi usiku na mchana ili jengo hilo linaloendelea kujengwa liweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo lenye ghorofa nane lilitakiwa kukamilika Mwezi huu Disemba, 2020 lakini mpaka sasa limefikia asilimia 41. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati) akiangalia paa la ghorofa ya tatu ya jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji linaloendelea kujengwa jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, leo. Amemtaka Mkandarasi wa Meadi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kulikamilisha jengo hilo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akiagana na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga, baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi unaoendelea wa Makao Makuu ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...