Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
BEKI wa Azam FC na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Aggrey Morris rasmi amestaafu kuchezea timu hiyo inayojiandaa kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2021) Mashindano yatakayofanyika nchini Cameroon mwezi huu wa Januari.Kwa siku nyingi, Morris ameitumikia Timu ya Taifa katika Michuano mbalimbali sambamba na kuisaidia kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2019) Michuano iliyofanyika nchini Misri kwa mara ya kwanza tangu kufuzu mara ya mwisho 1980.
Kwa Aggrey Morris hakuna ubishi ameisaidia Taifa Stars ndio maana tunasema yeye ni Alama isiyosahaulika katika Soka la Tanzania haswa Timu ya Taifa. Unakumbuka Mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda (The Cranes) mchezo uliopigwa dimba la Uwanja wa Taifa kwa sasa Uwanja wa Benjamin Mkapa?
Hapa tunakumbuka Tanzania kufuzu AFCON 2019 nchini Misri, katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Uganda, Aggrey Morris alifunga bao tatu la mchezo, na kuifanya Tanzania kufuzu AFCON kwa mara ya kwanza tangu 1980 kwenye mashindano yaliyofanyika nchini Nigeria.

Katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya DR Congo, Aggrey Morris ameagwa katika timu ya taifa wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bushungwa akimkabidhi hundi ikiwa ni sehemu ya zawadi ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars” kwa muda wote.
Si hiyo tu bali hata, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega amemkabidhi Morris Mpira uliosainiwa na Wachezaji ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars.”
Haikuishia hapo pia, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia alimkabidhi Aggrey Morris jezi iliyosainiwa na Wachezaji, benchi la Ufundi na viongozi ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...