BILIONEA mtanzania kutoka wilayani Simanjoro Mkoa wa Arusha Saniniu Laizer amekabidhi Shule ya Msingi  yenye vyumba Saba ,nyumba za walimu mbili pamoja na matundu ya vyoo 10 kwa uongozi wa serikali ya wilaya hiyo chini ya mkuu wake wa wilaya Zehania Chaula .

Shule hiyo ambayo imepewa jina lake la Saniniu imejengwa katika Kijiji Cha Naepo kilichopo kata ya Naisinyai wilayani humo ambapo imetumia zaidi ya shilingi milioni 466 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya shule hiyo wilayani humo Bilionea Laizer aliaza kwa kuishukuru familia yake kwa ushirikiano ambao wanaendelea kumpatia huku akiishukuru serikali kupitia wizara ya elimu katika kumuunga mkono na kumkubalia kujenga shule hiyo na kuipa jina lake.

Laizer amesema kazi hiyo haikuwa nyepesi kwani ni kazi ambayo inahitaji uzalendo ,upendo thabiti dhidi ya Taifa lake lakini kubwa zaidi kujitoa hivyo anashukuru kwa kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ambayo kimsingi aliaza kuijenga mwaka 2017.

"Ndugu zangu leo najisikia fahari kubwa kukabidhi shule hii ambayo kwa asilimia 95 imekamilika na palipobakia ni sehemu ndogo ambapo naamini kwa kushirikiana na serikali tutakamilisha "amesema Laizer

Nakuongeza kuwa " amejenga vyumba sita vya madarasa kwa shilingi milioni 158,matundu ya vyoo 10 kwa shilingi milioni 26 nyumba za walimu mbili kwa maana 2 in 1zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa thamani ya shilingi 187 lakini pia vyoo ,jiko ,ukuta kwenye nyumba za walimu kwa thamani ya shilingi milioni 46 namshukuru sana Mungu."amesisitiza Laizer

Pia ameongeza kuwa atahakikisha eneo lililobakia ambalo ni la ujenzi wa bwalo ,jiko,uzio stoo,vinakamilika na kutokana na ushirikiano uliopo Kati ya serikali na yeye Kama mchimbaji wa madini ambaye ameamua kurudisha sehemu ya faida kupitia kile anachokipata.

Katika hatua nyingine Bilionea Laizer ameipongeza wizara ya madini kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia hali ambayo imewezesha kufikia hatua aliyonayo na kwamba ataendelea kushirikiana na serikali katika  kuunga mkono juhudi zake kadri atakavyokuwa anabarikiwa .

Amesema ujenzi wa shule hiyo umegharimu gharama kubwa kutokana na udongo wa eneo hilo lakini pia imejengwa katika kiwango chenye ubora wa hali ya juu ambacho kinakidhi matakwa ya shule husika.

"Nimalize kwa kusema ndugu mgeni rasmi kazi hii haikuwa nyepesi Kama nilivyosema awali nikazi ambayo inahitaji  moyo thabiti hususani katika kushirikiana na Jamii inayonizunguka .na ahadi yangu nitaendelea kujitoa kadri Mungu atakavyojalia."amesema Laizer

Kwaupande wake mwakilishi wa mkuu wa wilaya hiyo ambaye ni Katibu tawala Zuwena Omary kwaniaba ya serikali amemshukuru Laizer kwa kujitoa kwake na kumwahakikishia kuwa wao Kama serikali wataendelea kumpa ushirikiano.

Amesema kuwa alichofanya bilionea huyo ni cha mfano  na uzalendo mkubwa na Kuna haja ya watanzania wengine kuendelea kushirikiana na serikali nakwamba atafikisha shukrani zake kwa serikali.

muonekano wa shule ya msingi Saniniu ambayo Kwa asiliami 95 imekamilika na imejengwa na bilionea huyo mtanzania Saniniu laizer .
Bilionea Saniniu Laizer akizungumza mbele ya viongozi wa Wilaya hiyo wakati wa makabidhiano ya  shule ambayo imepewa jina lake .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...