Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba SC, Sven Vandenbroeck ameachana na timu hiyo kwa kile kilichoelezwa ni makubaliano ya pande zote mbili kati yake na Klabu hiyo iliyofuzu hatua ya Makindi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hapo jana dhidi ya FC Platinum.

Taarifa iliyotolewa na Simba usiku huu imeeleza kuwa Bodi yake imewataarifu Mashabiki na Wanachama 

Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza kushukuru kwa mchango wa Sven kwa kipindi chote alichokuwa na Simba SC ikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania, Kombe la FA na Kombe, Ngao ya Jamii na kuifikisha timu Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa imeeleza Kocha Msaidizi, Suleiman Matola atachukua timu katika Kipindi hiki hadi pale atakapotangazwa Kocha mwingine atakayerithi mikoba yake. Pia Simba inamtambua Sven kama Mwanafamilia na kumtakia kila la kheri katika safari yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...