Na Mwandishi wetu, Simanjiro
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Haki Madini la jijini Arusha, limewajengea
uwezo wachekechaji wanaochekecha udongo ndani ya ukuta unaozunguka
migodi ya madini ya Tanzanite, kwa kuwapatia elimu ya namna ya kujikinga
na madhara yatokanayo na shughuli wanazofanya.
Ofisa
miradi wa shirika la Haki Madini, Emmanuel Mbise akizungumza kwenye
kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro amesema lengo ni kuwajengea
uwezo zaidi wa kufanya kazi katika mazingira salama.
Mbise
amesema katika kufanya kazi za uchekechaji inatakiwa kuvaa vifaa vya
kujikinga na vumbi ili kuondokana na ugonjwa wa kifua kikuu na ulanga
kuingia kwenye kifua.
"Wakati
wa kuchekecha muwe mnamwagia maji katika udongo ili vumbi lisiingie
vifuani na kwenye mapafu kisha kupata TB na Silikosisi kupitia vumbi na
ulanga unaokuwepo wakati wa kazi," amesema Mbise.
Amesema
kufanya kazi kwa muda mrefu hujenga majeraha kwenye baadhi ya viungo
vya mwili na mifupa hivyo tunapaswa kupumzika kila baada ya kzii na
kufanya mazoezi.
"Pia
kwenye shughuli zetu hizi za uchekechaji wa madini tunapaswa kupumzika
ili kuupa mwili nafasi kwani madini yapo tuu yanatakiwa yatupe faida na
yasituathiri," amesema Mbise.
Ofisa
mtendaji wa kata ya Naisinyai, Valentine Tesha amewataka wachekechaji
hao 60 waliopatiwa mafunzo hayo wawe mabalozi wazuri kwa kutoa elimu
waliyoipata kwa wengine ambao hawakuipata.
Tesha
amesema washiriki hao wakisambaza elimu hiyo kwa baadhi ya wachekechaji
ambao hawajafika kwenye mafunzo hayo watakuwa nao wamejengewa uwezo.
Mmoja
kati ya wachekechaji hao, Isaya Maliyaki amesema wamekuwa wakitoa elimu
waliyoipata kwa baadhi ya vijana wachekechaji ila hawatekelezi.
Maliyaki
amesema baadhi ya vijana walevi wanawaeleza kuwa watumie vifaa vya
kujikinga vumbi kwa kuvaa barakoa lakini hawatekelezi hilo.
Mwenyekiti
wa wachekechaji ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite, Nai Leyani
amelishukuru shirika la Haki Madini kwa kuwapa elimu hiyo kwani kwa
namna moja au nyingine imewasaidia.
Leyani
amesema wamekuwa wakiwapa elimu baadhi ya wachekechaji wenzao ambao
hawajapata mafunzo hayo hasa wanawake ambao wamekuwa wanatekeleza hayo
kwa kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi na kumwagia maji mchanga.
Meneja miradi wa shirika lisilo la kiserikali la Haki
Madini Emmanuel Mbise akizungumza na wachekechaji wanaochekecha ndani ya
ukuta unaozunguka madini ya Tanzanite.
Wadau wanaochekecha migodi ya madini ya Tanzanite wakiwa
kwenye mafunzo ya usalama kazini yaliyotolewa na shirika lisilo la
kiserikali la Haki Madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...