********************************************

30/01/2021 DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Polisi Wasaidizi waliopo kwenye taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia sheria sambamba na nidhamu wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku katika kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya kikao kazi na Polisi Wasaidizi waliopo Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa, weledi, ufanisi na kujituma kutasaidia kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii wanayoihudumia.

Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, uwepo wa Polisi Wasaidizi umesaidia kuwezesha mamlaka na Halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kuendelea kuimarika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...