Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, Bakari Kimwanga na mwenzake wa Mzimuni Manispaa ya Kinondoni, Manfred Lyoto wamebaini uchafuzi wa mazingira katika mfereji wa mpaka unaotenganisha kata zao.

Katika ziara yao walioifanya leo madiwani hao wakiwa wameambatana na wenyeviti wa mitaa ya Mtambani, Abdullah Kitumbi na Ibrahim Mselemu wa Kimamba, walikagua mfereji huo ambao walibaini nyumba nyingi za zilizopo kando ya mfereji huo, zimeunganisha mabomba ya maji machafu ikiwamo kutiririsha maji taka.

Akizungumzia hali hiyo Diwani Kimwanga, amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho mvua zipo jirani ni lazima mfereji huo usafishwe kwa kuwashirikisha wananchi.

"Ni aibu kwani yapo mambo ambayo wenyeviti wa mitaa mnatakiwa kuuangalia badala ya kukaa ofisini. Hivyo leo tumeona namna baadhi ya wananchi wameunganisha mabomba ya maji taka jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

"Tunachoomba wenyeviti kutaneni haraka mpange kikao cha pamoja ambacho kitashirikisha wananchi wa pande mbili na hiki kikao mtuarifu mapema mimi na mwenzangu (Lyoto) tutahudhuria," amesema Kimwanga

Kwa upande wake Diwani Lyoto, amesema kuwa ipo haja kusafishwa kwa mfereji huo ikiwamo kuomba nguvu ya pamoja kwa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni.

"Yapo maeneo yanahitaji nguvu Kazi ya wananchi na mengine ni lazima tusafishe mfereji kwa kutumia burudoza," amesema Lyoto







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...