Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akijibu hoja mbalimbali
mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, zilizoulizwa na Kamati hiyo,
jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Suleiman Kakoso,
akifafanua jambo kwa viongozi wa
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya
Ujenzi), pamoja na wajumbe wa kamati yake wakati wa uwasilishwaji wa taarifa
mbalimbali za miundo na majukumu yaliyo chini ya Sekta hiyo, jijini Dodoma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle,
akiwasilisha taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Wakala huo kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.
Kuhusu ujenzi wa karakana katika kila wilaya, Mhandisi Maselle, amesema kuwa tayari TEMESA imenunua karakana zinazotembea (mobile workshop), kwa karakana ambazo zipo nje ya miji na kukarabti zile zilizochoka ili kurahisisha huduma kwa wateja wao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Suleiman Kakoso, amesema kuwa ili
wakala huo uweze kusimama na kujiendesha kibiashara Serikali inatakiwa
itoe fedha kwa wakala huo.
Ameiagiza Wizara kupitia TEMESA na Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA), kuwasilisha mchanganuo wa madeni wanayodai
katika taasisi zote za Serikali kwa Kamati hiyo ili kuweza kusaidia kusukuma na
kukumbusha Serikali kulipa madeni hayo.
Ameitaka pia Taasisi ya Teknolojia
ya Ujenzi (ICoT), kuendelea kujikita katika utoaji wa elimu kwa ngazi ya
chini ili kupata wataalamu kama mafundi sanifu na mafundi mchundo ambapo kwa
sasa wataalamu hao wanaonekana kupungua.
TEMESA, TBA, Vikosi vya Ujenzi pamoja na
ICoT ni baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi ambapo leo
zimewasilisha taarifa zao kuhusu miundo na majukumu yao kwa Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambapo pamoja na mambo mengine Taasisi hizo
zimetakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuleta tija kwa Taifa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...