Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na
wanufaika wa TASAF (hawapo pichani) Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui,
Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF Kijiji cha Kinamagi Wilayani
Uyui, Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwahimiza wanufaika wa TASAF
Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora kutumia vizuri
ruzuku wanayoipata ili kuboresha maisha yao na kuondokana na umaskini,
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia) akimsikiliza mnufaika
wa TASAF, Bi. Zena Hussein wa Maganga wa Kijiji cha Kinamagi Wilayani
Uyui, Mkoa wa Tabora akielezea mafanikio aliyoyapa kupitia TASAF,
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwatazama mbuzi wa mnufaika
wa TASAF Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Bi. Zena
Hussein Maganga alipomtembelea mnufaika huyo ili kujionea mafanikio
aliyoyapata wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ziara yake ya kikazi yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, mara
baada ya Naibu Waziri huyo kumaliza zoezi la kuwatembelea wanufaika wa
TASAF katika Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi na mnufaika wa TASAF, Bi. Enviolatha Gerald Kamage mbele ya
nyumba ya mnufaika huyo ambaye ametumia ruzuku aliyoipata kujenga
nyumba hiyo, kununua cherehani, sola na kuweka umeme wa REA.

WANUFAIKA wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanaopokea ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wamekumbushwa wajibu wa kuboresha maisha yao kwa kutumia vizuri fedha za ruzuku wanazopatiwa ili kuondokana na umaskini.

Akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewaasa wanufaika kutotumia kwa anasa ruzuku inayotolewa na TASAF na badala yake waitumie katika shughuli za maendeleo kama kilimo, ufugaji na ujasiriamali.

Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, ni wajibu wa kila mnufaika kuhakikisha anajiinua kiuchumi kupitia fedha inayotolewa na TASAF, kwani Serikali kwa upande wake inaendelea kutekeleza wajibu wake na maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuziwezesha kaya zote maskini nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Mhe. Ndejembi amewataka wanufaika wa TASAF kutosita kujikwamua katika umaskini kwa kuhofia kuondolewa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, na badala yake wajisikie fahari kuondokana na umaskini na hatimaye kuwa mfano bora wa kuigwa na wanufaika wengine ambao hawakutumia vema ruzuku inayotolewa na TASAF.

Aidha, Mhe. Ndejembi amezitaka Serikali za Vijiji kuacha kudai tozo ndogo ndogo kama za ujenzi wa shule siku ambayo wanufaika wanapokea ruzuku, kwani tozo hizo zinawakwamisha wanufaika kutumia ruzuku wanayoipata kwa ajili ya shughuli zitakazowasaidia kujiondoa katika umaskini.

Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata kutokata ruzuku za wanufaika kwa ajili ya kuchangia huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwani wanakwamisha jitihada za wanufaika kuboresha maisha yao, hivyo amewataka kuwaacha wanufaika wazalishe fedha ndipo wachangie huduma za mfuko huo.

Mara baada ya kuzungumza na Wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Kinamagi, Mhe. Ndejembi aliwatembea wanufaika ili kujionea maendeleo waliyoyapa na hatimaye kushuhudia maendeleo ya Bi. Enviolatha Gerald Kamage ambaye ametumia vizuri ruzuku kununua cherehani, kujenga nyumba, kununua sola na kuweka umeme wa REA.

Mhe. Ndejembi ameshuhudia pia, maendeleo ya mnufaika wa TASAF, Bi. Zena Hussein Maganga ambaye amefanikiwa kutumia vema ruzuku kwa kufuga mbuzi, kuku, kununua mbolea kwa ajili ya kilimo ikiwa ni pamoja na kununua sola inayowawezesha watoto wake kujisomea wakati wa usiku.

Madhumuni ya utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini ni kuziwezesha kaya hizo kuboresha maisha kwa kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi, malazi, huduma za afya na mahitaji ya wanafunzi shuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...