*Atoa ufafanuzi sakata la Mkude

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAR IN DAR ni Hamasa iliyowekwa  na Simba SC ili kutia nguvu ndani ya dakika 90 kwa wachezaji, kuona hakuna lingine ni kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mashabiki wa Soka nchini haswa wa Simba SC wameombwa kufika Uwanjani kwa wingi na kuhakikisha wanaimba WIDA! WIDA! WIDA! ili kushinikiza ushindi kwa timu yao katika mchezo wake wa mkondo wa pili dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe, mchezo utakaopigwa Januari 6, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hayo yameendelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo, Haji Sunday Manara alipozungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye mchezo huo wa marudiano.

"Sisi Simba SC mtaji wetu mkubwa wa ushindi ni mashabiki wetu kujaa Uwanjani, tunaamini wakija kwa wingi watawapa hamasa Wachezaji wetu kucheza kwa kujituma na kupata ushindi katika mchezo dhidi ya FC Platinum." amesema Manara.

Manara amesema tayari Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeridhia mchezo huo uchezwe majira ya Saa 11 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki ili kutoa nafasi zaidi kwa Mashabiki wa Soka hususan wale wanaotoka sehemu za mbali.

"Majibu ya barua kutoka CAF wameridhia mechi ichezwe Saa 11 Alasiri, CAF walipanga mchezo uchezwe Saa 1 usiku, kwa upande wetu tulisema hapana lazima tuombe Saa 11 ili kuwapa nafasi mashabiki wetu kushuhudia mchezo huo kutokana na Miundombinu ya mji wetu wa Dar, hulka za Mashabiki, mwisho wa siku tuwape nafasi mashabiki mkurejea kwao mapema", ameeleza Manara.

Amesema Simba SC imeiandika barua CAF kuhusu suala la kujaza mashabiki katika dimba la Benjamin Mkapa kwa asilimia 100 ya uwezo wa Uwanja huo, amesema hawatauza tiketi kwa asilimia zote 100 ya idadi ya uwanja hadi CAF watakorudisha majibu ya ruhusa ya kujaza Uwanja huo wa Benjamin Mkapa.

SAKATA LA MCHEZAJI JONAS MKUDE LIKOJE?


Haji Manara amesema tayari suala la Mkude lipo kwenye Kamati ya nidhamu ya Klabu hiyo ya Simba, bado linasubiri majibu,

 "Jonas Mkude ni sehemu na wachezaji wa Simba SC hajafukuzwa Simba SC lakini ni taratibu tu za Klabu zimewekwa na yeye ameridhia". Amesema.

Pia amesema maamuzi yatakapofanywa na Kamati ya nidhamu Mchezaji huyo atarejea kujiunga na wenzake Kikosini. Amesema Mkude ndiye Mchezaji mwandamizi katika Klabu ya Simba akitimiza miaka 10 mfululizo bila kuhamia sehemu nyimgine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...