Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mjumbe wa Baraza
la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kabla ya kuanza
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita
leo tarehe 08 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji Saini wa mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Masanja Kungu Kadogosa na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC kupitia Mtendaji Mkuu wa CCECC Zhang Junle katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mjumbe wa
Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakati
akizungumza mara baada ya utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR
kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli
Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil
Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction
Corporation Limited CRCC katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu
ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakati wakielekea kupata chakula cha mchana katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akiongoza
mazungumzo kwa upande wa Tanzania pamoja na Ujumbe wa Kutoka China
uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika Ikulu ndogo
ya Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mara baada ya
kuzungumza na wageni mbalimbali katika hafla fupi ya utiaji saini wa
Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga
km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za
Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China
Railway Construction Corporation Limited CRCC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wadogo wadogo wamachinga na kuwapa zawadi Waandishi wa Habari waliokuwepo katika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo kuhusu
zawadi ya Kinyago cha mti wa Mpingo kwa Mjumbe wa Baraza la Taifa na
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ili akiwasilishe kwa Rais wa
China Xi Jinping mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake hapa
nchini.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
China Wang Yi katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...