RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa 
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria 
kuifungua Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusini 
Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya 
Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. 
Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid 
Hadidi Rashid na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali 
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba
 Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman .(Picha na 
Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa 
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwalimu wa 
Somo la Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa
 waKusini Unguja na (kuia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na 
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said na Katibu Mkuu wa 
Wizara hiyo Dkt. Idrisa Muslim Hija, akitembelea Maabara ya Skuli hiyo 
baada ya kuifungua leo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya 
Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa 
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa
 Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said alipowasili 
katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni, kwa 
ajili ya ufunguzi wa Skuli hiyo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha 
Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar na (kushoto kwa Waziri) Makamu wa Pili
 wa Rais wa Zanzibar Mstaaf Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Katibu wa Baraza 
la Mapinduzi  na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri
 wa Nchi  Afisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora 
Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS
 wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali 
Mwinyi akiondoa kipazia kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya 
Sekondari ya Hasnuu Makame Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja na (kulia) 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.HemedvSuleiman Abdulla na Waziri 
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na 
Ikulu).
                                        
                                        
                                    
        
        
        
 



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...