RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizindua Kalenda Amani
Milele, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Amani
lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar
na (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Waandishi waliopata Elimu ya Amani
Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Sheria Katiba
Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na
Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika
ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar
lililoandaliwa na Friends of Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar beach resort Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid, Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Nchi
Afisi ya Rais Sheria,Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.
Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kalenda ya Amani
Milele baada ya kuizindua katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa
Kongamani la Pili la Amani lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach
Resort na (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Waandishi wa habari waliopata
mafunzo ya Amani Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais
Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali
Suleiman.(Picha na Ikulu)
MUFTI Mkuu wa DRC – Congo Sheikh
Abdalla Luamba Mangara akitowa Salamu za Friends of Zanzibar wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar uliofanyika
katiuka ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Jijini
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa Serikali wakifuatilia
ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar, wakati Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali
Mwinyi (hayupo pichani) akilihutubia na kulifungua katika ukumbi wa
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini wa kwanza Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Mahmoud Mussa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan
Othman.(Picha na Ikulu)
BALOZI wa Norway Nchini Tanzania
Mhe.Elisabeth Jacobsen akitowa salamu ya Nchi yake wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na
Friends of Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort
Mazizini Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa
Norway Nchini Tanzania Mhe,Elisabeth Jacobsen akitowa salamu wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Amani Zanzibar lililofanyika katika
ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Zanzibar na kuandaliwa na Friends of
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais
Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali
Suleiman, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa
Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of
Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini
Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)WAJUMBE
wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na
Friends of Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)
lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Zanzibar.(Picha na
Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...