Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amekutana na
kufanya kikao na Wawakilishi wa Wazee wa Mkoa huo kwa lengo la
kusikiliza changamoto zinazowakabili Wazee ili Serikali iweze kuzifanyia
kazi.
Katika kikao hicho RC Kunenge amepokea changamoto na
mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wazee hao ambapo zipo changamoto
zililizopatiwa majibu ya papo kwa papo na nyingine za kisera na kisheria
ambazo ameahidi kuzifikisha katika ngazi husika.
Aidha RC
Kunenge amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa Mkoa huo kwa kazi
kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kueneza Busara, hekima na maarifa kwa
jamii Jambo linalosaidia kuwa na kizazi kinachofuata maadili na kulinda
amani na usalama mkoani humo.
Hata hivyo RC Kunenge amewaeleza
Wazee hao kuwa ofisi yake iko wazi kupokea na kusikiliza ushauri kutoka
kwa Wazee na ataweka utaratibu kukutana na Wazee wa Mkoa huo kila baada
ya miezi mitatu.
Pamoja na hayo RC Kunenge amewasihi Wazee
kuendelea kuwa kisima Cha maarifa na kuhakikisha wanakuwa washauri
wazuri wa Amani, Upendo, upatanisho na watoe nasaha kwa jamii.
Kwa
upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho wamemshukuru RC Kunenge kwa
namna anavyowakumbuka na kuwathamini Wazee wa Mkoa huo na wamemuahidi
watampatia ushirikiano wa kimawazo Katika kila Jambo.
WAZEE NI HAZINA, PALIPO NA WAZEE HAKUNA KINACHOHARIBIKA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...