*Simba wakabidhiwa Kombe kibingwa, Luis Miquissone aibuka mchezaji bora wa mechi
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KASI,akili, uwezo , umaridadi na kila aina ya ufundi ulitawala katika mchezo wa kibabe iliowakutanisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam dhidi ya timu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR.
Mchezo huo ulianza saa 11 jioni, katika Uwanja wa Mkapa huku maelfu ya mashabiki wa soka wakishuhudia mtanange huo ambao umezikutanisha timu hizo kupitia mashindano ya Simb Super Cup ambayo ndio mara ya kwanza kufanyika nchini baada ya uongozi wa Klabu ya Simba kuamua kuanzisha mashindano hayo.
Wakati mchezo ukiendelea mashabiki wa Simba waliokuwa wengi uwanjani hawakuwa nyuma kuishangalia timu yao,huku mashabiki aa TP Mazembe nao wakionesha kuwa na matumaini na timu yao.
Kadri dakika zilivyokuwa zikiendelea na hasa katika dakika 15 za mchezo huo TP Mazembe walionekana kusuka mipango lakini umakini wa wachezaji wa Simba ulisaidia kuvuruga mbinu na mipango ya wapinzani wao.
Dakika za kipindi cha kwanza ziliendelea kwenda huku macho ya mashabiki yakishuhudia burudani ya aina yake kutokana na soka safi lililokuwa likichezwa.Hata hivyo dakika 45 za kipindi cha kwanza kilikamilika bila goli,nyavu zilitulia tuliii.Refa wa mchezo huo Matinyi Sanya aliongeza dakika mbili kufidia muda uliopotea kutokana na mchezo kusimama.
Vikosi vya timu zote mbili ilikuwa hivi; Kikosi cha Simba kilianza na Benno Kakolanya, David Kameta, Mohamed Hussein, Pascal Wawa, Joash Onyango, Tadeo Lwanga, Miraji Athumani,Rally Bwalya, Mutshimba Kope Mugalu, Claatous Chita Chama pamoja na Luis Miquissone.
Wachezaji wa akiba ni Ally Salim( mlinda mlango) Gadiel Michael, Mzamiru Yassin, Middle Kagere,Ibrahim Ajibu,Bernard Morrison Kennedy Juma, Francis Kahata, Lukosa Junior, Peter Mduhwa pamoja na Perfect Chikwende.
Wakati kwa upande wa timu yaTP Mazembe ilianza na Mounkoro Ibrahim, Arsene Zola Kiaku,TindiMwape, Kabaso Chongo, Joseph Ochaya, Chris Kisangala ,Christian KoffiKoume, Freddy Joel Djedje ,Isaac Tshibangi, Rainfolrd Kalaba pamoja na Moustapha Kouyate.
Kwenye benchi la akiba walikuwepo Sylvain Gbohouo,Mputu Tresor, Guy Stephane Bedi, Patou Kabangu,Martial Zemba, Thomas Ulimwengu ,Mayombo Etienne Raby,Binemo Le Beau, Sudi Bibonge Gondri,Gode Masengo Gamba,Nicolas Kazadi pamoja na Aime Kabula Ulonde.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa utulivu mkubwa kutokana na kila timu kusoma mchezo wa mwenzake kutokana na aina ya mpira uliochezwa kipindi cha kwanza.Timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu huku walimu wa pande zote wakifanya mabadiliko kwa wachezaji ,ikiwa ni sehemu ya kuimarisha safu za ulinzi na ushaumbuliaji.
Hata hivyo hadi mpira unamalizika hakuna mbabe kwani hakuna aliyefanikiwa kupata bao. Hivyo Simba na TP Mazembe wamegawana sare ya alama moja kwa moja.Kutokana na matokeo hayo Simba ametangazwa kuwa bingwa wa michuano ya Simba Super Cup kwani amefikisha alama nne na magoli manne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...